Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC), Clifford Tandari akifafanua jambo wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari lililofanyika mapema leo kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Bw. Tandari alieleleza lengo kubwa la kukutana na Wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ni kuwaeleza na kuwafanya watambue fursa na mchango wa Kituo cha Uwekezaji wa kunadi miradi ya uwekezaji, Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala mazima yanayohusu uwekezaji na kuwahudumia wawekezaji kwa mtindo wa “One Stop Centre”. 

"Kama sote tunavyofahamu uwekezaji nchini umechangia kwa kiasi kikubwa sana kukuwa kwa uchumi wetu. Nchi ambayo haivutii wawekezaji na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara kamwe haiwezi kufanikiwa katika uchumi wake. Kubwa zaidi ni kwamba Tanzania inashindana na nchi zingine zote duniani katika kuvutia wawekezaji hao hao, hali ambayo inatuhitaji kuwa makini zaidi na jinsi tunavyowahudumia wawekezaji wa ndani na wale wa nje wanaotaka kuja kuwekeza nchini mwetu" alisema Bw. Tandari.

Bw. Tandari alisema kuwa TIC kwa sasa imejipanga katika kuandaa mpango mkakati ambao utaweza kurahisisha Utekelezaji wa majukumu ya Kituo na kusimamia utekelezaji wa maagizo na malengo yake, Alisema kuwa wanaamini mpango mkakati huo utarahisisha Usimamiaji wa shughuli na mipango yao na kwamba wanategemea mpango mkakati huo utaweza kusaidia Kituo kuhakikisha Utekelezaji wa Majukumu yao unaendana na mahitaji ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC).Clifford Tandari akifafanua mambo mbalimbali kuhusiana na sula zima la uwekezaji hapa nchini wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari lililofanyika mapema leo jijini Dar.

Bw. Tandari alieleza kuwa Kituo cha Uwekezaji kina mkakati maalumu wa kuhakikisha upatikanaji wa Sera na Sheria Mpya ya Uwekezaji kwani ile ya awali imepitwa na wakati. "Sera yetu ya Uwekezaji pamoja na Sheria vimepitwa na wakati na haviendani na mazingira ya sasa na tupo kwenye taratibu za kufanyia marekebisho sera na sheria ili kuhakikisha vinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya nchi yetu katika masuala yanayohusu Uwekezaji"alisema Bw. Tandari.

Alisema kuwa Vivutio vingi wanavyopewa wawekezaji vinalenga kuwapa nafasi ya kuanza kuzalisha bidhaa zao mapema na hivyo kuwa na uwezo wa kulipa kodi katika muda mfupi zaidi. "Kwa misingi hii kivutio kikubwa kuliko vyote ni huduma wanayoipata kutoka serikalini kuwa bora, ya haraka na isiyo na ukiritimba unaozaa usumbufu mkubwa kwa wawekezaji. 

"Mkakati wa Serikali ni kukiwezesha Kituo chetu kuboresha huduma bora chini ya “One Stop Shop” kwani ni muhimu sana katika kuondoa usumbufu kwa wawekezaji na kujenga mazingira bora ya uwekezaji kwa wote. Mwekezaji hana haja ya kuzunguka ili kupata vibali mbalimbali. Badala yake Anapata huduma ya vibali hivi kupitia Kituo Cha Uwekezaji" alisema Bwa.Tandari .
Meneja Mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Pendo Gondwe akiratibu mijadala iliokuwa ikiendelea wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.
Baadhi ya Makaimu Wakurugenzi wa TIC wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...