Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefungua kitabu cha maombolezo kwa ajili ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa walioko nchini kutoa salaam zao za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee ABOUD JUMBE MWINYI. 

Kitabu hicho kitakuwa wazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Albert Luthuli, Dar es salaam kuanzia leo siku ya Jumanne Agosti 16 hadi Ijumaa Agosti 19, 2016 toka saa 4 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Mzee ABOUD JUMBE ambaye pia alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki dunia juzi nyumbani kwake Mji Mwema, Kigamboni, Dar es salaam na kuzikwa jana katika makaburi ya Migombani Unguja, Zanzibar.

Wana-diplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kutoka Finland, Msumbiji, Burundi, Uganda na Angola tayari wameweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.

Mzee JUMBE alishika madaraka ya kuongoza Zanzibar mwaka 1972 baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume baada ya Baraza la Mapinduzi kumchagua kwa kauli moja. Kutokana na kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar mwaka 1984, Mzee JUMBE alilazimika kujiuzulu na viongozi wengine.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam

Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland Bw. Simo Pekla Parvianen akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. 


Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Bi. Monica Patricio Mussa akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. 
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Elitrea Bw. Saleh Azaril 
Kaimu Balozi wa Burundi nchini Tanzania Bw. Pierre Ndayishimiye 
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Angola Bw. Joel Cumbo .Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Selikarini, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...