Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Wananchi wa Rukwa wakiwa wameshika mabango ya kumkaribisha waziri Mkuu Mkoani Humo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wafipa wakati walipowasili kwenye kijiji cha Mtowisa mkoani Rukwa kuzungumza na wanachi Agosti 24, 2016. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa inatarajiwa kupata huduma ya maji safi na salama kuanzia mwezi ujao baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliokuwa unajengwa.

Mradi huo unajengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Manispaa ya Sumbawanga (SUWASA), kwa ufadhili wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani kupitia benki yake ya Maendeleo (KfW), sh. bilioni 31 utakapokamilika.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana  (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati na akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga na kuitaka kampuni ya kampuni ya Techno Fab Gammon Joint Venture ya India kumaliza ujenzi wa mradi huo haraka iwezekanavyo.

Amesema mradi huo ambao tayari umekamilika kwa asilimia 85 unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na Manispaa katika kulinda miundombinu ya mradi huo mara utakapokamilika pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

“Pamoja na Serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini,changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo imekuwa kubwa kutokana na baadhi ya visima vimeanza kukauka hali inayosababishwa na uharibifu wa mazingira,” amesema.

Amesema kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya vyanzo vya maji ambapo wananchi wanajishughulisha na shughuli za ulimaji, uchungaji wa mifugo, ujenzi wa nyumba za makazi na uchomaji misitu hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira na hatimaye vyanzo hivyo hukauka.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wote wa wilaya na wenyeviti wa vijiji nchini kuyasimamia maeneo yenye vyanzo vya maji na kuwaondoa watu wotewalioyavamia kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Naye Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye alimuwakilisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge katika hafla hiyo alisema aliishukuru Serikali ya Ujerumani na Umoja wa nchi za Ulaya kwa kufadhili mradi huo.

Hata hivyo Mhandisi Kamwelwe alisema suala la kuhifadhi mazingira ni msingi endelevu wa upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo aliwaomba wananchi kujiepusha na uchafuzi wa vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira ili kuepuka athari ya Taifa kukubwa na janga la ukame.

“Wananchi wanatakiwa kuacha kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kulima, kufuga ndani ya mita 60 kutoka katika mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji ili kuepusha uharibifu wa mazingira ambao madhara yake ni makubwa kwa viumbe wote,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...