Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam  

Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.

Bi Shakila alifariki jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa taarabu hakuwa anaumwa wajati mauti yanamkuta.

KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MOLA akulaze pema Peponi Kipenzi chetu Bi Shakila Saidi. Amen.

    ReplyDelete
  2. Hivi hakuna picha ambazo aliwahi kujistiri mkaweka kaka michuzi eeh!

    ReplyDelete
  3. Umeuliza la maana mdau wa 2. Mini nadhani hawa wanahabari wetu wanahitaji mafunzo zaidi katika fani yao hiyo ya habari maana ni muhimu kujuwa picha ya aina gani inaendane na habari gani na mazingira gani, hilo bado ni tatizo, mana wanaweza kuweka picha ikamdhalilisha muhusika bila wao kujali.

    Pumzika kwa amani Pema Peponi Daima Milele Bi Shakila Saidi. Amin.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...