Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia chips na kutengeneza mikorogo.

Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hii inatisha kweli, tuko salama na mafuta haya?

    ReplyDelete
  2. Ndani ya Ziwa Victoria Ktk visiwa vya wavuvi, nywele za binadamu hutu mika kukaushia samaki!

    ReplyDelete
  3. Kwani kabla ya kupigwa marufuku yalikuwa yanaruhusiwa kutumika? Nilidhani polisi badala ya kuwafuatilia original comedy na minguo inayofanana nao wangewakama hao watumiaji wa mafuta ya transforma ambayo yanaua watanzania wengi kila siku. Lakini wenzetu polisi wanaipa kipaumbele vitu vidogo vidogo.

    ReplyDelete
  4. ndio maana kasi ya kansa imezidi Tanzania. Tunatumiaje mafuta ya transfoma wakati mafuta ya alizeti hayana cholesterol na yanapatikana kwa bei nafuu??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...