WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekagua vifaa na maeneo yatakayotumika kwa ajili ya tiketi za kieletroniki
zitakazoanza kutumika Septemba Mwaka huu.
                    
 Nape amekagua maeneo hayo pamoja na mitambo itakayokuwa inatumika kwa ajili kukagua tiketi za mashine zikiwa kwenye hatua ya mwisho za umaliziaji na Septemba 04 utakabidhiwa kwa Wizara hiyo ili kuanza kutumika.

Mashine hizo zitasaidia katika kuongeza mapato kwa timu pamoja na serikali huku kukiwa na utaratibu wa kutumia kadi zitakazokuwa zinatumika kama ATM itakayotumika kulipia tiketi.

Hatua hiyo itaweza kupunguza ulanguzi wa tiketi pamoja na tiketi feki zilizokuwa zikiuzwa kiholela.
Waziri wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akielekea katika uwanja wa Taifa kukagua mashine za Kieletroniki zitakazo anza kutumika kuanzia Septemba mwaka huu akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Elisante Ole Gabriel akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye  akipata maelekezo alipoingia kwenye chumba chenye mashine za Kieletroniki jijini Dar es Salaam leo.
Hatua za mwisho za umaliziaji wa ufungaji wa mashine za Kieletroniki katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...