Na Fredy Mgunda,Mufindi.


MBUNGE wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa amekabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi, zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo iliyopo Kijiji cha Mdabulo wilayani mufindi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Mdabulo, alisema kuweza kujenga jamii imara ni lazima kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele cha pekee.

“Sina budi kuunga mkono juhudi zenu za ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mdabulo, ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, nami kama mwakilishi wetu ninaungana nanyi kwa dhati na katika hili napenda kukabidhi mifuko ya saruji.huo.Alisema lengo la kutoa msaada huo, ni kutokana na shule hiyo kuwa chakavu katika maeneo muhimu kama kwenye mabweni na bwalo ambalo hutumiwa na wanafunzi kwa ajili ya chakula.

“Baada ya kupata taarifa hizi, nimeamua kuja na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi ili waangalie namna ya kufanya marekebisho katika madarasa pamoja na mabweni ya shule hii na nimewaagiza wahakikishe wanakarabati shule hiyo na iwe kwenye viwango vinavyotakiwa,” alisema Mgimwa.Mgimwa aliwataka wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufaulu na si kusoma ili kupata ajira kama ilivyozoeleka kwa watu wengi kwani serikali inafahamu changamoto ya ajira iliyopo.

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema huku wakisaidiana na walimu kwa kushirikiana katika nyanja ya elimu ili kupanua wingo wa ufaulu kwa wanafunzi.“Kwa kipindi cha siku kadhaa nimekuwa na ziara katika katika jimbo langu kwa lengo la kutimiza ahadi zangu pamoja na kusikiliza kero ya wananchi na kero moja wapo ni wazazi kutowajali  wanafunzi wala kutojua maendeleo ya watoto wao pindi watokapo shule”alisema Mgimwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Geogrge Mgomba, aliwataka wanafunzi wake kusome kwa ajili ya ajira binafsi na si kutegemea ajira kutoka serikalini kwa kuwa serikali ina mzigo mkubwa.“Wanafunzi mnatakiwa msome kwa bidii na msitegemee ajira kutoka serikalini, mtafute ajira binafsi au kujiajiri wenyewe,”alisema



Kwa upande wake,mkuu wa wilaya ya mufindi Jamhuri Wiliamu, alimshukuru mbunge huyo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi za kuinua sekta ya elimu katika wilaya hiyo.
MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akihutubia wananchi waliofika kwenye mkutano uliyafanyika kwenye shule ya sekondary Mdabulo. 
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini mahamood mgimwa
 MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akikabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo kwa uongozi wa wilaya ya mufindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...