Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Elimu, Sayansi
 na Teknolojia
  Dkt. Leonard Akwilapo
Na Lilian Lundo - MAELEZO 
 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaukumbusha Umma kuwa mitihani ya Taifa ya Darasa la 4 na Kidato cha 2 itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida. 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akikanusha taarifa za kutokuwepo kwa mitihani hiyo kwa mwaka 2016. 
“Napenda niukumbushe Umma kuwa mitihani hii ni muhimu sana katika ufuatiliji wa maendeleo ya wanafunzi wetu. 
"Kwa hiyo mitihani yote miwili itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida. Kama kuna watu wanawaambia kuwa haitafanyika wawapuuze kabisa,” alifafanua Dkt. Akwilapo 
 Dkt. Akwilapo aliendelea kwa kusema kuwa mitihani hiyo ina umuhimu mkubwa katika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa lengo la kufanya maendeleo ya kitaaluma. 
Aidha kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajafikia viwango vya ufaulu vilivyowekwa watatakiwa kukariri darasa au kidato. 
 Amebainisha kuwa Baraza la Mitihani ndilo lenye jukumu la kushughulikia maandalizi ya mitihani hiyo ikiwa ni pamoja na utungaji, uchapaji, ufungaji na usafirishaji hadi ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa na majukumu ya kuhakikisha kuwa uendeshaji na usahihishaji wa mitihani hiyo unafanyika kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...