JIJI la Dar es Salaam linatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa awamu ya nne wa hoteli za Africa ambapo wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wapatao 200 wanatarajiwa kuhudhuria kuzugumzia masuala muhimu katika sekta ya ukarimu.

Mkutano huu umeandaliwa na kuratibiwa na kampuni ya kimataifa ya LNoppen na HD Partnership ambapo wameingia katika makubaliano ya kuandaa mkutano huu. Wadau na wamiliki wa hoteli wanaweza kuhudhuria katika mkutano huu kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba kupitia tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya LNoppen Group amesema, “ Tanzania ni nchi iliyo juu kwa kutembelewa na wageni mbalimbali kutoka barani Afrika na mataifa mengine. Kampuni nyingi za kimataifa zimewekeza nchini Tanzania na nchi inazidi kuimarika katika kanda ya Afrika. Tumeona ni vyema mkutano wa mwaka huu tuufanye nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo hapa hasa katika sekta ya Utalii na Ukarimu”.

Nchi zilizoandaa mkutano huu katika miaka iliyopita ni Ghana 2014, Sengal 2015 na Nigeria Januari 2016.
Katika siku mbili za mkutano huu mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ukarimu na utalii yatajadiliwa ikiwa pamoja na usimamizi wa mapato, marejesho ya mtaji, rasimali watu na ajira, huduma bora kwa wateja na ushindani katika sekta ya Utalii Afrika. Majadiliano yatafanyika katika paneli ambapo tafiti zitajadiliwa kwa kina. Mkutano utafunguliwa na Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye atatoa utambuzi wa sera za serikali na vichocheo kwa wawekezaji nchini Tanzania.

Akiongelea umuhimu wa Mkutano huu, Meelis Kuuskler, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HD Partnership amesema, “ Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa namna hii, mkutano huu hautatangaza Tanzania kama kitovu cha Utalii peke yake bali utatangaza nchi kwa wawekezaji na jumuiya ya maendeleo kwamba Tanzania ipo wazi kwa biashara''
Wadau mbalimbali wa sketa ya Utalii na Ukarimu wanasisitiziwa kuwa watapata fursa ya kuhudhuria mkutano kwa kujiandikisha kabla ya tarehe 6 Septemba 2016. Kujiandikisha na kupata taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya africa.hotelandresortsummit.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...