Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza, Arusha
Mchimbaji
wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa
Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani.
Akithibitisha
kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani
baada ya kuwasha moto wa mkaa ili kulainisha mwamba ili aweze kupata maji kwenye kisima chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha.
"Kilichotokea
ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa
ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika. Mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda. Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...