Polisi Konsitebo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Sharifa Ismaili akikabidhi mipira kwa moja ya timu zilizofanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo ya MPINGA CUP 2016, makundi raundi ya kwanza kutoka kundi C iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kitunda, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam.
Staff Sajent wa Polisi, Enock Machunde akifundisha jambo kwa madereva wa Boda boda wakati wa michezo ya Mashindano ya MPINGA CUP 2016 kundi C zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Eric Ndidi akitoa mipira kwa timu za kundi C zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam (Picha na Traffic Makao Makuu).
Na: Traffic Makao Makuu.
MASHINDANO ya Kombe la MPINGA CUP 2016 hatua ya makundi
inayoendelea kwenye Mkoa wa Kipolisi Ilala iliyopangwa kwenye makundi sita tayari
makundi matatu yamekamilisha ratiba baada ya kupata washindi wa michezo yao ya
awali kutoka kundi C, timu hizo zimechuana kuwania nafasi ya kusonga hatua ya
pili baada ya jana kukamilisha ratiba hiyo na kuwa kundi la tatu kuungana na
kundi A na B ambayo michezo yake imeshakamilika.
Mchezo wa kwanza wa kundi C ulianza majira ya saa nne
asubuhi katika Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi ikiwa ni siku ya Jumamosi
tarehe 27/8/2016 ambapo timu ya Chakenge F.C iliweza kucheza dhidi ya timu ya
Mara fc ikifuatiwa na Mchezo wa pili ambao timu ya Kivule C.C.M (A) ilipata
Ponint za mezani baada ya timu ya Polisi Kitunda kushindwa kutokea Uwanjani na
kukabidhiwa Mpira mmoja kwa ajili ya kujinoa kwa kinyang’anyiro cha mzunguko wa
pili.
Mchezo mwingine ilikuwa ni kati ya timu ya Mwembeni Fc
Kivule iliyoshindwa kutumia vyema nafasi walizopata kipindi cha kwanza ambapo
waliambulia kupata goli 1 dhidi ya wenzao wa Amani fc wakati timu ya Matembele
Kivule walishinda kwa kupata magoli mawili (2) katika mchezo wa tatu huku
mchezo wan ne (4) Njia Panda Msikitini fc Kitunda ilitolewa kwenye mashindano
na timu ya Relini Kitunda iliyoibugiza kwa jumla ya mabao 3-2 na kuzawadiwa
mpira ili wakajiweke vema na mzunguko wa pili.
Mwendelezo wa Mashindano haya ya MPINGA CUP 2016, ilifuata
siku ya 28/8/2016 Siku ya Jumapili na michezo iliyochezwa ilikuwa ni mitano (5)
ikiwa na jumla ya timu kumi zilizokutana kwenye kutafuta nafasi ya kusonga
mbele hatua ya kwanza mtoano, Katika Mchezo huo mgumu kwa timu zote mbili, Matembele
fc (KIPUNGUNI) dhidi ya timu ya Pentagini Fc ambapo mshindi alikuwa ni
Matembele Kipunguni kwa njia ya Penalt -4-3 na kuzawadiwa mpira kwa ajili ya
kwenda kujiandaa na mchuano wa dulu la pili.
Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Kitunda fc Kivule
iliyocheza na timu ya Mwembeni fc Kivule
na timu ya kitunda Fc ilifanikiwa kuibuka na Ushindi wa mnono wa mabao 3-1
dhidi ya wenzao wa Mwembeni Fc na kuzawadiwa Mpira moja kwa ajili ya kwenda
kujiandaa na raundi inayofuata.
Na mchezo wa Tatu uliokuwa na mshikemshike mkubwa dhidi ya
timu zote kwa Mashabiki wao, Timu ya MACHIMBO F.C walifanikiwa kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MUSOMA BUCHA F.C MACHIMBO ambayo hata hivyo mchezo
huo ulimalizika kila timu ikiwa na mashike mshike mkubwa na ulikuwa ni mchezo
wa kusisimua kutokana na ulivyochezwa kwa ufundi mkubwa na wachezaji wa timu
zote mbili hata ivyo mshindi alizawadiwa mpira kwa lengo la kwenda kufanya
maandalizi mazuri ya mzunguko wa pili.
Michezo yote hiyo iliongzwa na Mafunzo Muhimu kwa Walimu wa
Masuala ya Elimu ya Usalama Barabarani ambao walitoa Mafunzo hayo kwa timu zote
kabla ya kuingia uwanjani huku wakifundidishwa pia Alama za Barabarani na
Kuulizwa Maswali na Washindi mbali mbali walizawadiwa Furana kutoka kwa
wadhamini Mbali Mbali wa Mashindano haya ya MPINGA CUP 2016 yanayofanyika
kwenye Mkoa wa Kipolisi ILALA.
Ambapo timu ya Kitunda Sabato Fc ilifanikiwa kuifunga timu
ya Kipunguni Relini kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo ambao ulikuwa wa
Upande mmoja huku wachezaji wa timu ya Kipunguni Relini wakisingizia Uwanja
kuwa na Michanga wakilinganisha na Beach Soccer, pamoja na yote lakini hatimaye
washindi walipatikana na kufnikiwa kijipatia zawadi ya mpira mmoja kila timu
iliyoibuka Kidedea.
Mchezo wa Mwisho Timu ya Kivule Silali ilipepetana na timu
ya Nyantila fc, timu mbili ambazo ni wapinzani wa jadi walijikuta wakimaliza
dakika 90 kwa kutoshana nguvu baada ya kumaliza wakiwa wamefungana bao moja kwa
moja 1-1. Lakini hata hivyo kutokana na Sheria ya Mashindano mshindi ni lazima
apatikane, walikwenda kwenye mikwaju ya Penalti na mshindi kuwa timu ya Nyantila
Fc waliopata mikwaju ya Penali nne (4) huku wenzao wa timu ya Kivule Silali
wakiambulia kupata mikwaju miwili (2) ya Penalti na hivyo kumaliza Kundi hilo
na Sasa Mashindano Haya ya MPINGA CUP 2016 yatafanyika Kiwalani wiki hii kama
ratiba inavyoonyesha.
RATIBA YA MASHINDANO YA BODABODA KUNDI D:
Uwanja ni Chuo cha Walemavu Kiwalani Tarehe 3/9/2016.
1. Mafundi Fc Vs PANDA KIWALANI F.C
2. BOMBOM F.C vs KIJIWE SAMLI KIWALANI
3. YOMBO HOSPT.KIWALANI vs MORNING STAR KIWALANI
4. KIPAWA FC vs KIPAWA SHELI FC
5. VINGUNGUTI SCANIA vs KIZOTA F.C VINGUNGUTI
6. MORNING STAR F.C vs WASHAWASHA F.C
7. KIWALANI BEACH F.C vs BODABODA GARDEN
KAtika UWanja huo huo tarehe 4/9/2016
1. VINGUNGUTI RELINI vs MAZIZI F.C
2. MTI PESA vs MASHUJAA F.C
3. TABATA DARAJANI F.C vs BALAKUDA HIGHLAND FC
4. GOGOVIVU F.C vs BODABODA F.C
5. MANDEZE F.C vs YOMBORELI F.C
6. VIPAJI FC vs GOLAN F.C
Inavyoonekana kwenye kundi hili kutakuwa na ushindani mkubwa
sana kutokana na timu nyingi kujitokeza kujiandikisha kutoka maeneo ya kundi D,
ambapo jumla ya 14 zitacheza siku hiyo ya jumamosi na siku inayofuata jumla ya
timu 12 zitacheza na kupata washindi pekee watakaosonga mbele hatua inayofuata
ya mashindano haya a kusisimua na yenye mafunzo mazuri kwa madereva wa Boda
boda.
Wadhamini mbali mbali wamejitokeza kudhamini na kuweza
kufanikisha michezo hii kuwa ya aina yake mwaka huu ikiwa ni pamoja na Udhamini
Wa G.S.M wauzaji wa Piki waliotoa zawadi ya Pikipiki kwa Mshindi, Cool Blue
Tanzania ambao kwa hakika wameonyesha Sapoti nzuri kwa kutuhakikishia Maji kwa
wachezaji wakati wote wa michezo sambamba na kampuni ya Coca Cola,Big Bon, NMB,
Zantel, Haki Elimu, Star Times, Windhoek, Red Bull, NHIF, PUMA, Yono, Dar City
Promotions, TBL, Milcom, E.F.M Radio, T-Marc Tanzania, Michuzi Blogs, Mwananchi
Communications, Dira Tv, My Way Entertainment, Mashujaa Band, MpaluleBlogs:
Miss Demokrasia Tanzania, Balozi wa Demokrasia Tanzania, na Jeshi la Polisi
Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...