Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.
 Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa..
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Na John Stephen.
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO imeanza upasuaji kwa watoto wanane na wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula ili kuwa sawa na watu wengine ambao hawana matatizo hayo.

Madaktari wa hospitali hiyo wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Misri ambao wamewasili leo wakitokea Misri kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo. 

Madaktari wa Muhimbili ni Dk. Zaitun Bokhary, Dk. Yona Ringo Madaktari, Dk. Herman Wella, Dk. Victor Ngolta, Dk Mwajabu Mbaga, Dk. Joachim Angela, Dk. Hashim Lituli na Dk. Gertrud Mollel wakati madaktari  na wataalamu wa kada nyingine kutoka Misri ni Mahamed Malak, Saber Waheeb, Amr Alaa, Tamer Ghoneim, Ragia Mohamed Awad, Sherouk Saad Ayoub, Hazem Ahmed.

Wataalamu hao wametembelea watoto waliolazwa kwenye Jengo la Watoto na kujadiliana na madaktari wa hospitali hiyo jinsi watakavyotoa huduma za upasuaji kwa watoto hao.

Kwa mujibu wa Dk Julieth Magandi, watoto wengine sita watafanyiwa upasuaji huo kesho.  Dk Magandi amesema Leo madaktari hao wameanza kwa mtoto mwenye tatizo la mfumo wa chakula na hewa  na kwamba watoto pacha wawili waliungana na kutenganishwa kutoka Mbeya nao watafanyiwa upasuaji wa kuweka sawa mfumo wa njia ya mkojo.

Baadhi ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni; Nasra Rashidi, Hughes Khalid, Fahad Selemani, Elikana Joel, Eliudi Joel, Hasna Hamis Kalemea,  Ibrahim Haji na Sofia Ramadhani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...