Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania Alphonce Felix Simbu (24) leo ametia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku
ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Alitumia saa 2:11:15, sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne Ghirmay Ghebreslassie.
Mkenya Eliud Kipchoge ndiye aliyeibuka mshindi na kunyakuwa medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume. Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 na  kushinda medali ya fedha huku Mmarekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ndugu zetu wa Kenya wana medali kibao. Sisi Watanzania tumeridhika na nafasi ya tano.

    ReplyDelete
  2. Ha Ha Ha! Tanzania bana! Sasa aliyetia fora ni nani? Aliyekuwa wa kwanza ama wa tano?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Has we uelewi?katia fora kwa Tanzania. .maana hatujawahi kushika nafasi hiyo. .Eee TZ masikini sijui sisi tunaweza nini, si mpira,wala kukimbia ni porojo tu..na tumeisharidhika na hali hiyo. .ndo maana hata asili mali zetu watumia majirani kujitangaza. .sisi tumezidi kwa uzuzu. .tumebakia music na drama za tv

      Delete
  3. Nakubariana na mwandishi wa hii taarifa ni kweli ametiafora......nilikua natazama live mwanzo mpaka mwisho kwakweli amejitahidi sana. Mwandishi amezingatia mambo mengi kabla ya kuandika mojawapo likiwa historia yetu ktk ushiriki wa mashindano makubwa kama haya na nafasi tunazoshika. Huyu Simbu naamini kabisa atakuja kututoa kimasomaso 2020 Japan iwapo atapewa msaada wa kutosha na wananchi wote wenye mapenzi ya kweli kama mwandishi wa habari hii. Ni matumaini yangu kwamba atapokewa kwa heshima kubwa mara atakaporudi nyumbani.

    ReplyDelete
  4. Sidhani kama tumeridhika, sema tu lisilobudi hutendwa maana hatuna namna wala jinsi. Ila tusife wala kuvunjika mioyo, alau kajitahidi hakuwa wa Dhahabu, Fedha wala Shaba, lakini pia kaonyesha jitihada zake nafasi ya tano pia tushkuru kuliko asingetokezea kabisa! Binafsi nakupongeza sana Alphonce Felix SIMBU usivunjike moyo abadan, endelea na mazowezi tena kwa ari kabisa ili panapo uhai na uzima ukatuwakilishe vizuri zaidi huko Tokyo. In Sha Allah.



    ReplyDelete
  5. Winning a lot of medals depend on how much you invest in each and every game to your athletics. Rich countries are the one with most medals. So guys stop blaming Tanzania!

    ReplyDelete
  6. Mimi binafsi namponeza ndugu yetu Alphonce kwa kuipeperusha bendera yetu japo hakupat medali amejitahidi. Tuwape moyo wenzetu wanapothubutu na kujaribu badala ya kuwakatisha tamaa.

    ReplyDelete
  7. Duh hii hatari ametia fora ya wapi? ameshika nafasi ya tano. Aliyetia fora ni wa nafasi ya kwanza. Huyu hakupata medali yeyote.

    ReplyDelete
  8. I think the earlier comments are missing the point which is the recognition and encouragement that this post is after.
    Hongera kwa mwanariadha wetu. Keep it up :)

    ReplyDelete
  9. It's a shame that we even sent a team. Our standard ought to be clear and simple. Once we begin winning against our best performing neighbors- Kenyans, Ethiopians, South Africans, then should we begin venturing far afield. Otherwise it's sheer lunacy .

    ReplyDelete
  10. Jamani huyu jamaa ni mshindi kuliko hata wa Kenya. Wakenya kila siku wanapata, lakini huyu jamaani mi mara ya kwanza kushiriki na ameshika na 5 kati ya watu 160!!!!!!! yaani hiyo ni big surprise

    ReplyDelete
  11. Let us support him. Amejitahidi sana ukitilia maanani ni mara yake ya kwanza kushiriki. Kushika nafasi ya 5 kati ya watu 200 is not a joke.

    ReplyDelete
  12. NDUGU ZANGU Watanzania nini Kenya iliwafanyia? Mwatuogopa nini? Wale wamarekani mnaowaona hapo juu Wa Silver, na nambari sita na saba huja kufanya mazoezi Kenya.
    Tumeni wana riadha wenu Kenya waje wafanye mazoezi, mahali pa kuishi kwa kambi mtapewa, mtakula ugali, sukuma , nyama na maziwa kwa wingi. Njooni Iteni, Nyahururu mfanye mazoezi ya riadhaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...