Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameendelea na ziara yake Mjini Ugunja na kutembelea taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Bank kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar na Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyopo chini ya Wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya uwasilishwaji wa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank kuu tawi la Zanzibar, na Naibu Gavana wa Bank hiyo Dkt. Natu Mwamba, Bw. Mansour Abdalla Meneja wa fedha na utawala wa Bank hiyo tawi la Zanzibar alieleza kuwa dhana ya ajira kwa watumishi wa Bank hiyo kwa ni ya upendeleo na kujuana haina ukweli wowote kutokana na sababu kuwa taratibu ajira za Bank hiyo zimewekwa pamoja katika makao makuu ya Bank hiyo jijini Dar es Salaam na huwa nafasi za kazi hutangazwa katika magazeti na wananchi wenye vigezo kupata kazi.

“wananchi wajenge tabia ya kusoma magazeti hasa kwa wale wanaotafuta ajira katika bank hii kwani kazi za hapa huwa zinatangazwa huko na bank inatoa ajira bila upendeleo na kwa upande wa Zanzibar asilimia 48% ya watumishi ni wazanzibari na asilimia inayobakia ni ya upande wa pili wa Muunano.” Alisisitiza Bw. Mansour.

Akitolea ufafanunuzi suala la mgawo wa asilimia 4.5% ya mapato ya Bank hiyo kwa Zanzibar kama sehemu ya Muungano, Mkurugenzi wa Fedha wa Bank hiyo Tawi la Zanzibar bw. Jamhuri Ngelime alisema kuwa hana Jibu la moja kwa moja kuhusu mgao huo ila serikali hizi mbili za muungano zilikubaliana kuwa asilimia 45% ya faida ya Mapato yote ya Bank hiyo nchini igawiwe kwa Zanzibar, na hivyo sheria ndiyo inavyosema.

Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina, aliitaka Bank hiyo kufanya bidii ili kuhakikisha inafikia malengo ambayo serikali imejiwekea, na kuishauri bank hiyo kuongeza huduma zake za ki bank hasa kwa upande wa Pemba na kuweka masharti nafuu kwa wafanya biashara wenye ma bank, ili kuweza kutoa huduma hiyo na kuondoa gape ya kifedha iliyopo kati ya Unguja na Pemba.

Wakati Huo Huo, Naibu Waziri Mpina aliitembelea Tume ya Sayansi na Teknolojia tawi la Zanzibar COSTECH na katika majadiliano na watumishi wa tume hiyo Naibu Wazri Mpina alisema kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu sana kwa nchi yoyote duniani kuendelea, nchi haiwezi kuingia kwenye Biashara ya Gas na oil bila wana sayansi kufanya tafiti zao.

Na kupongeza mchango wa taasisi hiyo katika jamii, ikiwa ni pamoja na kufadhili wanachuo wanasansi mbali mbali nchini.


Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Unguja ilihusisha kutembelea taasisi za Muungano, Kumuwakilisha Mhe. Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi alipozaliwa Makamu wa Rais, Pamoja na Kutembelea Ofisi zake zilizopo Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alieyesimama katikati ni Naibu Gavana wa Bank Kuu tawi la Zanzibar Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank hiyo kwa upande wa Zanzibar kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, menejimenti ya Bank Hiyo na Ujumbe wa Naibu Waziri, haupo pichani, Ulipotembelea taasisi hiyo ya muungano, aliyekaa kushoto ni Bw. N. K. mboje Mkurugenzi wa Tawi hilo kwa upande wa Zanzibar.
Anayeongea kwa vitendo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Bank Kuu tawi la Zanzibar mara baada ya kutembelea taasisi hiyo ya muungano mjini Unguja. 
Bi Safia Hashim, Mtengenezaji na Muuzaji wa mapambo na sabuni zitokanazo na zao la mwani, mdau anayefadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH taasisi ya muungano iliyopo chini ya wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania tawi la Zanzibar, akimuelezea Naibu Waziri Mpina faida na matumizi ya zao la mwani na kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho yaliyoandaliwa na taasisi hiyo mjini Unguja wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi watumishi wa tume ya sayansi tawi la Zanzibar. COSTECH alipotembelea taasisi hiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar. (Picha zote na Habari na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)

EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
HABARI KUTOKA ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...