Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza Hospitali zote nchini kuweza kufanya ukarabati wa vifaa vyote vya Mahospitali yao ambavyo wamerundika stoo, ili kusaidia kupunguza gharama za manunuzi ya vifaa vipya ambavyo ni gharama kubwa.


Dk. Kigwangalla ameyasema hayo Wilayani Meatu, Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo amepongeza juhudi za Hospitali ya Meatu kwa hatua yao ya kuamua kufanya ukarabati wa vifaa vyote vya Hospitali hiyo huku wakiokoa mamilioni ya fedha.

“Napongeza Hospitali ya Meatu kwa ubunifu huu waliofanya. Kwani wameweza kuokoa mamilioni na hii napenda kutoa maagizo kwa Hospitali zote hapa nchini kuhakikisha wanakarabati vifaa hivyo ambavyo vingi wamekuwa wakirundika tu stoo kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza gharama.” Amesema Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.

Hospitali hiyo ya Meatu imeweza kufungua kalakana ya kufanyia matengenezo na ukarabati wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda vya wagonjwa pamoja na vifaa vingine vingi ambavyo kwa manunuzi yake ni gharama kubwa sana.

Naibu Waziri huyo pia amepata kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo ikiwemo sehemu za Mahabara, Chumba cha upasuaji, wodi ya Wakinamama, kitengo cha meno, mapokezi na bohari ya chanjo ya Wilaya pamoja na duka la dawa la wilaya hiyo ndani ya Hospitali huku akikuta mapungufu kadhaa ambayo amwaagiza wawe wameyashughulikia ndani ya miezi mitatu kabla ya kuchukuliwa hatua thabiti pindi watakapokiuka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akishuhudia baadhi ya vitanda vya Hospitali vilivyofanyiwa ukarabati.
Baadhi ya vitanda vilivyofanyiwa ukarabati
Vitanda vya kujifungulia wodi ya wazazi.. ambavyo inaelezwa kuwa kitanda kimoja kina gharimu zaidi ya milioni moja na nusu

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa baadhi ya vitanda vya Hospitali vilivyofanyiwa ukarabati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...