Taarifa iliyotufikia usiku huu inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa kwa Askari Polisi wanne na raia kadhaa kujeruhiwa  lililotokea huko Mbagala Mmbande


jijini Dar.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.
Inadaiwa kuwa majambazi hayo  hayakuingia ndani ya benki. 
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa  kwa risasi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha na kusema: "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi".
-------------------------------------------
"Usiku huu nimefika Mbande-Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka  kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.
Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."

Mwigulu Nchemba
23.08.2016





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. asante sana kwa taarifa kaka!!

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa. Sidhani kazi ya kulinda Mabenki ni ya polisi. Mabenki waaajiri security company na waweke camera. Kazi ya security ni kuwashitua polisi kama kuna ujambazi na polisi wawe haraka kuja kupambana nao. Kuwaweka polisi usiku kucha kulinda tena nje ni sawa na death penalt. Ni rahisi kuwa ambushed na kuuwawa kwa sababu majambazi wanakuwa tayari wamesoma mienendo na taratibu zao za ulinzi. It is time to change the system!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesema vema sana. Kwa nyakati hizi ambapo benki zilizokuwa za taifa zimebinafsishwa, haikufaa kuwabebesha jukumu hilo askari wetu. Bali inapotokea uhitaji kama ilivyo kwa mazingira mengine.

      Delete
  3. Huzuni kubwa. Lakini pia ni kwa sababu ya kusema kuna watu wapewe mafunzo makubwa ya kivita wasubiri vita. na wengine wapewe mafunzo laini. Sasa hivi majambazi wanakuja kivita, kwa nini polisi wasiwe makomando?

    Au serikali ifute majeshi mengine, iongeze idadi ya jw, halafu wapangiwe kazi za polisi, magereza, zimamoto, uhamiaji, tanapa, nk.

    ReplyDelete
  4. Pale Dk Magufuli aliposema police wanatakiwa kujihami kabla hawaja dhuriwa na majambazi wanasiasa uchwara wa siasa za majitaka kama kawaida wakaanza kuleta siasa zao za kipuuzi sasa leo watoe ufafanuzi zaidi juu ya maisha ya hawa asksri waliopoteza maisha. kauli zao za kijinga na za kubeza kuhusu muheshimiwa raisi hii ndio faida yake. Tanzania hatuna wanasiasa wa upizani isipokuwa mashaka tu. Ni watu wanaoweza kuliingiza taifa katika maafa wakati wowote kama tahadhari isipochukuliwa.

    ReplyDelete
  5. Audhubillah
    Ndugu yangu hapo juu aomba kazi za kipolisi zichukuliwe na jeshi.Kwa lugha ya kigeni hii inaitwa Militarisation of the police force. Mungu wangu,pisha mbali janga kama hilo.Silaha za kivita ni za vita, na tekiniki ya civilian policing ni tofauti na za kijeshi. Kwa ufupi (pardon my French) ndugu aomba raia wawef... like by an army of occupation.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana,Dunia sijui inaenda Wapi na kwanini waue tu,waondoke!!

    ReplyDelete
  7. Poleni sana mliofikwa na maafa hayo, kwa kweli inasikitisha sana.
    Halafu ni kwa nini hizo picha zilizofatia hazina maelezo ili tungefaham na ingetupa wigo mpana zaidi wa kuchangia maoni yetu vizuri mana hivi hivi bila kupata uhakika wa wahusika pichani na kinachoendeleam basi inakuwa ngumu ku comment chochote. Au mmefanya makusudi.

    ReplyDelete
  8. Mambo gani haya, idara husika ifanye uchunguzi wa kina kubaini wahusika wa tukio hili baya na la hatari dhidi ya maafisa wa kulinda usalama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...