Na Theresia Mwami  TEMESA
 Wananchi wa Pangani na Bweni mkoani Tanga wamepata kivuko kipya cha MV. Tanga, ambacho sasa kitasaidiana na MV. Pangani II kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni.
Akiongea na wananchi wa Pangani Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase amesema  kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Tanga ni muendelezo wa sera ya Serikali ya kuboresha huduma ya vivuko katika maeneo mbalimbali yaliyo na mahitaji ya vivuko nchini.
“TEMESA imejipanga kuhakikisha kuwa vivuko vyake vyote vinafanyiwa matengenezo ya kinga kwa wakati, ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi wanaotumia vivuko hivyo inapatikana kwa wakati muafaka” Alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi Manase ameongeza kuwa  hivi sasa MV. Pangani II itakwenda kwenye ukarabati mdogo na baada ya ukarabati huo vivuko vyote viwili vitabakia katika eneo la Pangani na Bweni ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Lazaro Vazuri  alisema kuwa kivuko cha
MV. Tanga ni mwanzo wa uboreshajji wa huduma ya vivuko nchini na kwa sasa wapo katika mikakati ya kukarabati vivuko vilivyopo na kujenga vivuko vibya ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vivuko katika maeneo yenye huhitaji.
Mmoja ya wananchi wa Wananchi wa Pangani/Bweni Bw. Othman Juma Ali ameipongeza Serikali kwa juhudi za kupambana na changamoto ya vivuko inayozikumba sehemu nyingi zilizozungukwa na maji.
“Tumekipokea kivuko cha MV. Tanga kwa furaha kubwa na tunaiomba Serikali kutoa huduma ya kivuko hiki kwa saa 24  kila siku ili kitusaidie wananchi hasa wa eneo la Bweni kupata huduma hiyo nyakati za usiku tunapohitaji kupata huduma za kijamii upande wa Pangani” alisema Bw. Othman.
MV. Tanga imesanifiwa na kutengenezwa na Kampuni ya kitanzania ya Songoro Marine Company Ltd na kivuko hiki kina uwezo wa kubeba tani 50 ambazo ni sawa na kubeba abiria 100 na magari 6 kwa pamoja.
 Kivuko cha Pangani II pamoja na kivuko kipya MV. Tanga vikiwasili katika eneo la Pangani Jijini Tanga. 
 Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili katika eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.
  Abiria na Magari yakiingia kwenye  kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa huduma eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga. 
Baadhi ya wasafiri wakishuka katika kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa huduma eneo la Pangani na Bweni Jijini Tanga. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...