Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Tamasha la wasanii la kumuaga Mhr. Kikwete  baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma Julai 23, mwaka huu. 
 Shakila akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana
Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake  akiwa kwenye hafla hiyo
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 KAMANDA WA MATUKIO BLOG)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MOLA AKULAZE PEMA "SHAKILA BINT SAIDI" :

    Kubwa tushukuru MUNGU, na 'Fatiha' kupigia,
    Ila yatia uchungu, picha kiziangalia,
    Mwezi katu timu tangu, leo umetukimbia,
    PEMA MOLA AKULAZE, NASI NDIO KHATAMIA.

    Ghafula umetutoka, hakuna lotarajia,
    Si wa homa lalamika, wala tumbo ungulia,
    Lake MOLA kiandika, 'Fayakunu' latimia,
    PEMA MOLA AKULAZE, NASI NDIO KHATAMIA.

    Safari ilo ya kheri, YAILAHI kujalia,
    Lopituka kughufiri, adhabuze kwepushia
    Ya 'Munkari wa Nakiri', wepesi kukufanyia,
    PEMA MOLA AKULAZE, NASI NDIO KHATAMIA.

    Nuruye akuangaze, kivuliche kukutia,
    Jaza njema kuongeze, 'nari' yake kwepushia,
    Jannatuye akwingize, milele humo bakia,
    PEMA MOLA AKULAZE, NASI SOTE NDIO NJIA.


    "Kullu Nafsi Dhaiqatul Maut"
    "Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun"

    ReplyDelete
  2. Amin, Inna LILLAH wa Inna ilaihi Raajiuun,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...