Na Salum Mwinyimkuu, Morogoro.

Zaidi ya hatimiliki 300,000 za Ardhi zinatarajiwa kutolewa kwenye Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA mkoani Morogoro kupitia mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi wa LTSP, ili kupunguza Migogoro ya Mipaka kwenye Vijiji.

Miongoni mwa Changamoto inayofifiza Juhudi za Serikali kumaliza tatizo la Migogoro ya Ardhi katika Wilaya za KILOMBERO, MALINYI na ULANGA ni Rushwa kwa Baadhi ya Watendaji wasio waaminifu.

Wilaya ya KILOMBERO yenye vijiji 99 imejizolea Umaarufu kwa kuwa na maeneo mengi yenye Utata wa Ardhi,ikihusisha migogoro ya Mipaka baina ya kijiji na kijiji, hifadhi na kijiji pamoja na wakulima na wafugaji.
Godfrey Machabe Mratibu wa Program ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi (kushoto), Renit Halimba Diwani Viti maalum Wilaya ya Kilombero (wa pili kushoto) Lucas Mwaisaka Katibu tawala msaidizi Wilaya ya kilombero (kulia) Alicie Libenanga (wa pili Kulia) na Syabomi Mwaipopo (katikati) Dkt Steven Nindi Wakikabidhiana Mpango wa matumizi Bora ya Ardhi Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Wajumbe na Viongozi wa Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kushiriki Semina ya Uhamasishaji wa Ujenzi wa Masjala za Ardhi zaVijiji, Kukabidhi Mpango wa matumizi Bora ya Ardhi wa Wilaya na kutambulisha timu ya upimaji Mipaka iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.

Ili kuhakikisha Changamoto hiyo inabaki Historia, mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi umetua Wilayani Kilombero, ukiwa na Shabaha ya kupima mipaka ya Vijiji 20,na kupatiwa Hatimiliki ya Ardhi ili kuondoa Migogoro hiyo.

MARY MAKONDO ni Kaimu kamishna wa Ardhi nchini akizungumza Wilayani humo, ameeleza umuhimu wa Mradi huo unaofadhiliwa kwa Dola Milioni 15.2, wenye lengo la Kurasimisha Ardhi ili imnufaishe Mwananchi wa Masikini na kuondoa Migogoro isiyo na tija.

Zoezi hilo la Urasimishaji Ardhi na Utoaji wa Hatimiliki za Kimila litaenda sambamba na Ujenzi wa Masjala za Ardhi kwenye Vijiji vilivyopo kwenye mpango wa LTSP,lengo likiwa ni kuweka sawa kumbukumbu za Mikataba inayohusu Ardhi.

Itakumbukwa Mradi huu ni matokeo ya Mkutano wa wakuu wa nchi zenye Uchumi Mkubwa Duniani, ambapo Tanzania ilialikwa kuhudhuria kama mshiriki, ambako kulizinduliwa Ushirikiano kati yake na Kundi la G8 kuhusu uwazi kwenye sekta ya ardhi.
Kiongozi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Land Tenure Support Programme, Swagile Msananga akifafanua Jambo kuhusu Masjala za Ardhi za Vijiji katika Semina ya uhamasishaji wa Ujenzi wa masijala hizo iliyofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
Kaimu mkurugenzi mkuu tume ya taifa ya Matumizi ya ardhi Dkt Stephen Nindi (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Ardhi Bi Mary Makondo wakikabidhi mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya wilaya kwa kaimu Mkurugenzi wa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Gerald Kauki (Kulia) wakati wa Semina ya Uhamasishaji wa Ujenzi wa Masijala za Ardhi za Vijiji, Sambamba na kutambulisha timu ya upimaji Mipaka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Morogoro.
Timu ya Maafisa kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Waliosimama) iliyowasili Mkoani Morogoro kwa kazi ya Kupima na kumilikisha Ardhii takayofanyika katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...