Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete. 

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo. 


Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini. 

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza, 


“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi. 


Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo. 

Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo. 
Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari. NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza.
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...