Dar
es Salaam.
31/08/2016.
RAIS Dkt. John Magufuli
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
kongamano la tatu la kitaifa la afya
litakalofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 14-15 Novemba, mwaka
huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam Rais wa Taaasisi ya Tanzania Health
Summit (THS) Dkt. Omary Chillo alisema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa
na wadau 500 wa afya kutoka ndani na nje
ya Tanzania wakiwemo watoa huduma za afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa
ya afya, wachumi, na wadau wa maendeleo.
Alisema kongamano hilo
litalenga kuongeza nguvu za Serikali za kuboresha afya za Watanzania kupitia
kupashana habari na ujuzi, majadiliano ya changamoto na kufikia muafaka wa njia
bora za utatuzi wake ili kuimarisha huduma za afya nchini.
Aidha, alisema kuwa
mkutano huo utahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo vikao vya mashauriano
yatakayogusa mada mbalimbali za maendeleo ya afya, taarifa kutoka kwa wataalamu
wabobezi wa afya, pamoja na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.
Pia aliongeza kuwa katika
kongamano hilo pia kutakuwa na maonyesho ya huduma na bidhaa kutoka kwa
wasambazaji wa huduma za afya ya mashirika ya umma na binafsi.
Dkt. Chilo alitoa wito
kwa wadau wa afya nchini kutoka Serikalini, mashirika binafsi, mahospital,
asasi zisizo za kiserikali, taasisi za kitaaluma, wasambazaji, na washirika wa
maendeleo kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...