Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa Angela Kizigha.
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa
viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi
baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosis ya Kaskazini
Kati, Mchungaji Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la
Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na
Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na
viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira
ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo
nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya
Mungu.
Alisema kutokana na
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli
kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani halmashauri
zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo
yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali zitakazowawezesha
kufanya shughuli za uzalishaji mali, hivyo wawajulishe waumini wa dini
zote na serikali iko tayari kupanga
utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja
na madhehebu ya dini hii iwe inufaishe watu wote katika Mkoa huu bila kujali
itikadi za kidini wala kisiasa.
Askofu Stanley Hotay
aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya
ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na
changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani. Pia amependezwa nja
utaratibu huu kwa Mkuu wa Mkoa kuwatembelea viongozi mbalimbali wa dini ili kushauriana
masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wetu.
Aidha alishauri kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri
wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi
uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia
viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali
inayokusudia kuitekeleza ili watoe mawazo yao katika kuiboresha na kuifanya
itekelezeke kwa wepesi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...