Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akikagua timu wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars mkoani humo. Ameambatana na mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akipiga penati kufungua rasmi michuano ya Airtel Rissing Stars mkoani humo

Mwanza. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongella leo amefungua mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoani humo na kuwataka vijana kuzingatia nidhamu na taratibu zinazoongoza mchezo huo maarufu duniani.

“Hata ukiwa na kipaji cha aina gani bila kuwa na nidhamu kamwe huwezi kutimiza ndoto yako ya kuwa mchezaji nyota wa mpira wa miguu kwa sababu, kama ilivyo kwenye nyanja nyingine yoyote, mchezo wa soka unaongozwa na kanuni na sheria ambazo kila mchezaji lazima azifuate”, alisema.

Alisema kuwa binafsi anaifurahia sana programu ya Airtel Rising Stars kwa kuwa inakwenda sanjali na mikakati ya serikali ya kuwawezesha vijana. “Wote tunafahamu kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni chanzo cha ajira ya kuaminika kwa vijana duniani. Mnaweza kupata kipato na kuboresha maisha yenu kupitia mpira”, alisema Mongella na kuipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuwekeza katika soka kupitia programu hii ya vijana.

Alisema michuano ya Airtel Rising Stars inasaidia kubaini wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali ambao bila mashindano haya wangeweza kupotea hivi hivi. Aliwataka viongozi wa soka mkoa humo kushirikiana na shirikisho la soka nchini (TFF) kuwalea na kuwaendeleza vijana wanaopatikana kupitia Airtel Rising Stars.

Akiongea katika hafla hiyo ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Songora alisema kuwa Airtel Rising Stars imetoa hamasa kwa vijana wengi mkoani Mwanza kucheza soka na kuonyesha vipaji vyao. “Tunajivunia kuweza kutoa mfungaji bora na mchezaji bora katika fainali za mwaka jana. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni David Richard na Cypria Mtesigwa.

Songora pia alisema kuwa mkoa wa Mwanza umetoa wachezaji wa kutegemea katika timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys. Aliwataja wachezaji hao walioibuliwa kupitia Airtel Rising Stars kuwa ni Arish Suleiman, Cypria Mtesigwa, Ally Ng’anzi na Ally Hussein Msengi.

Kwa upande wake, Meneja wa kanda ya ziwa wa Airtel Tanzania Emmanuel Raphael alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Raphael.

Hafla hiyo ya ufunguzi ilishuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya Barass Sports Centre na Alliance Academy ambapo Barass Sports Centre waliwaduwaza wapinzani wao kwa kuwatandika 4-1. Mshambuliaji Frank Osoro alikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kufunga magoli huku goli la nne likifungwa na mlinzi wa Alliance aliyejifunga mwenyewe katika juhudi za kuutoa mpira katika hatari. Alliance Sports walipata goli la kufutia machozi kwa njia ya penati iliyofungwa na Rashid Hamis

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...