Serikali imeahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) inastawi na kufaidisha wananchi kwa kupitia miradi yake mbalimbali kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.

Akizungumza hayo katika uzinduzi rasmi wa TECC Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa watendelea kuwa pamoja na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya watanzania kiuchumi.

“Kwa niaba ya serikali natambua mchango wa wajasiriamali hivyo tupo pamoja na TECC kwa kila jambo watalofanya kwa ajili ya kusapoti uchumi wa nchi kupitia ujasiriamali katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mhe. Jenista

Mbali na hayo Mhe. Jenista amesema kuwa malengo ya TECC ni kuimarisha ubunifu na ushindani wa biashara ndogo na za kati za Tanzania kwa kuwavuta wajasiriamali waliopo ndani ya sekta isiyo rasmi, wahitimu wa vyuo na wengine wenye kutaka kuanzisha biashara zinazoongeza thamani kwa mazao na kutengeneza bidhaa nchini.

Aidha Mhe. Jenista amesema kuwa Biashara zikianzishwa nyingi na nyingi zikijipanua kiushandi ndivyo na serikali itapata mapato zaidi kupitia kodi hivyo uzalishaji uongezeke zaidi na zaidi kwa maendeleo ya nchi.

“Natoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiunga mkono TECC,” alisema, akiongeza kuwa fursa za kusaidia ziko nyingi kama kuwajengea uwezo kina mama wajasiriamali, wazee wanaostaafu, au kupanua programu ya Kijana Jiajiri katika mikoa mingine ya Tanzania.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TECC, Bi. Beng’i Issa alisema tangu kuanza kazi miaka miwili iliyopita, kwa kutumia rasilimali chache, taasisi hiyo imeweza kujipanga na kuonyesha mafanikio makubwa katika kujenga uwezo wa wananchi kumiliki uchumi.

“Tunahitaji kufanya zaidi ya hapa na uwezo huo tunao kama tutaungwa mkono na Serikali kikamilifu ili kuweza kutekeleza wajibu wa sera yetu katika kunyanyua wajasiriamali kwa maendeleo ya taifa,” alisema Bi. Beng’i

Aidha Bi. Beng’i amesema kuwa mpaka sasa TECC imeshatekeleza miradi miwili muhimu ambayo ni mradi wa Kijana Jiajiri ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Uingereza la Youth Business International (YBI) na kufadhiliwa na umoja wa makampuni yanayochimba gesi na mafuta katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Bi. Beng’i amesema kuwa Kupitia mradi wa Kijana Jiajiri na ufadhili wa shirika la International Youth Foundation ambalo limepata fedha kutoka Master Card Foundation vijana 1,250 watajengewa uwezo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma kuanzia mwezi ujao wa Tisa.

Kwa mujibu wa Bi. Beng’i, mradi wa pili ambao TECC imeufanya ni kwa kushirikiana na mradi wa BEST-Dialogue wa kufanya utafiti wa maoni ya wamiliki wa biashara ili kupata changamoto ambazo zinazuia ushindani kibiashara katika mradi wa Business Leaders Perception.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua na Meneja wa Ofisi wa TECC, Bi. Mwasiti Mkembe (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi kitabu cha Mpango Kazi wa miaka miwili cha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Bi. Beng’i Issa wakati wa uzinduzi rasmi wa TECC mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Beng’i pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bi. Beng’i Issa (wa pili kulia); mjumbe wa bodi hiyo, Dkt. Hassan Mshinda (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Bi. Issa pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakati Dkt. Mshinda pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Sehemu ya wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...