Na Bashir Yakub.

Iliwahi kuelezwa katika safu hii kuhusu aina mbalimbali za makampuni. Kubwa lililoelezwa ni kuwa unatakiwa kujua aina gani ya kazi/biashara unataka kufanya ili ujue ni aina gani ya kampuni itakufaa. Si kila kampuni inaweza kufaa katika unalotaka kufanya.

Na hii ndio sababu zikawepo aina mbalimbali za kampuni. Pia yafaa ujue kuwa kila aina yua kampuni utakayochagua inazo hasara zake na faida zake. Hata hivyo ili pawe na hasara itategemea uchaguzi wako wa kampuni kulingana na aina ya kazi unayotaka kufanya.

Makala ya leo yataeleza kampuni isiyo na hisa na kwa kazi gani kampuni hii inafaa . 

1.NINI MAANA YA KAMPUNI KUTOKUWA NA HISA.

Kampuni kutokuwa na hisa maana yake ni kuwa kampuni itakuwa kama kampuni nyingine zilivyo lakini haitakuwa na mtaji mkuu( share capital). Kawaida kampuni tulizozoea huwa zina hisa kwa mfano utasikia kampuni hii ina hisa 10000, au hisa 30000 au 100 nk. Katika kampuni ya aina hii hukutakwa na kitu cha namna hii.

2. JE INAWEZA KUWA NA WANAHISA.

Hapana kama haina hisa basi haiwezi kuwa na wanahisa. Hakuna mtu anaweza kujiita mwanhisa kama kampuni haina hisa. Itakuwa na wakurugenzi, katibu, na wanachama lakini sio wanahisa.

3. JE KUNA MGAO WA FAIDA KWA WANACHAMA.

Hapana kampuni ya namna hii haina mgawanyo wa faida (profit dividend) kwa wanachama wake. Hili halimaanishi kwamba kampuni hii haitakuwa ikilipa mishahara kwa wafanyakazi wake hapana. Katika uendeshaji wa kampuni kuna tofauti kubwa kati ya mgawanyo wa mapato na malipo ya mishahara.

Mgawanyo wa mapato huwa ni kwa wamiliki wa kampuni au wanahisa. Wakati mishahara huwa ni kwa wafanyakazi ambao pengine sio wanahisa au wamiliki wa kampuni. Mishahara huwa ni kwa waajiriwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...