Na Bashir Yakub.

Kampuni ya umma ndio huitwa public company kwa kiingereza. Kampuni hii hutofautishwa na kampuni binafsi (private company). Zote ni kampuni kwa ajili ya biashara na mara zote hutegemea unahitaji kufanya nini ili ujue ni kampuni ipi uunde.

1.JE KAMPUNI YA UMMA INAWEZA KUMILIKIWA NA WATU BINAFSI.

Ndio inawezekana. Watu wengi hudhani kwa kuwa jina la kampuni hii ni UMMA basi hudhani ni kampuni ambazo huundwa na serikali. Neno umma ni jina na limetokana na namna muundo wa kampuni yenyewe ulivyo , yumkini halina uhusiano wowote na kampuni za namna hii kumilikiwa na serikali.

Hivyo yafaa ifahamike kuwa hata wewe mtu binafsi mjasiriamali wa kawaida waweza kuunda kampuni ya namna hii pengine kutokana na faida zinazotokana na kampuni ya aina hii.

2.KWANINI UUNDE KAMPUNI YA UMMA BADALA YA KAMPUNI BINAFSI.

( a ) Uhuru wa wanahisa. Kampuni ya umma imetoa uhuru mkubwa kwa wanahisa. Wakati kampuni binafsi inaruhusu kuwa na wanahisa mwisho 50 kampuni ya umma haina ukomo wa idadi ya wanahisa.

Hii ina maana waweza kuwa na wanahisa hata milioni na zaidi. Hakuna ukomo wa kiwango cha mwisho isipokuwa kuna ukomo wa kiwango cha chini. Kiwango cha chini yalazimu wanahisa kuanzia wawili.

( b ) Uhuru wa kuuza na kununua hisa. Katika kampuni binafsi hakuna uhuru wa kununua na kuuza hisa. Katika kampuni binafsi yatakiwa kabla hujauza hisa zako kwa mtu mwingine upate ridhaa ya wanahisa wenzako. Wakikataa huwezi kuuza.

Lakini pia huwezi kumuuzia hisa mtu ambaye wanahisa wengine hawampendi. Yule wanayempenda na kumridhia ndiye huyo unayeweza kumuuzia tu na si vinginevyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...