Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha,Kitulo na Katavi.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete  alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanao tarajia kufika nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.

“ Wataaam na wanasayansi wa kitaifa na kimataifa wathibitisha kuwa  eneo pekee ambalo tukio hilo litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya nyanda za juu kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Katavi.Kitulo na Ruaha”alisema Shelutete .

“Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii”aliongeza Shelutete.
 
Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la rujewa wilaya ya mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.

Kwa upande wake mhifadhi wa idara ya  utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya tarifa za tukio hilo kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...