Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara  ambayo itaondoka  Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanza itakuwa Jumapili hii ya  Septemba 04, 2016 saa 9 alasiri. 
Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa  12 kutokea   Dar  es  Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika  stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa  mabehewa mawili mawili ya daraja la 3.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam. 
Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3 kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo  Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma za kuuzwa  tiketi za safari zake  mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba Mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kuto huduma hiyo kwa  wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani . Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za  behewa moja la daraja la 3. Mpango pia uko mbioni  wa  kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria. 
Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na wananchi kwa jumla nchini  hususan wale wa Mpanda na Kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari na huduma kuletewa karibu kwa kufuata sheria , taratibu na  kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliokusudiwa.
Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi ya treni ya Pugu na kufikia idadi ya behewa 18 hadi jana Agosti 22, 2016. Ni matarajio ya Uongozi ifikapo Agosti 31, 2016 treni hiyo ya Jiji  itakuwa na mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na ya jioni. 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Licha ya TRL kufungua kituo cha kukata tiketi mjini Kasulu,ni bora shirika likaingia katika teknolojia ya kukata tiketi kwa njia ya mitandao ya kipesa ili kuzima kabisa mianya ya rushwa. Stakabadhi za EFD zitumike kama ticketi.Shirika la reli ni moja ya mashirika lenye harufu ya rushwa hasa upande wa tiketi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...