Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), (wa tatu kulia), Mhe. Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa tano kushoto), Mhe. George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (wa nne kushoto), Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (wa kwanza kulia), Mhe. Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyemaliza muda wake (wa nne kulia), Mhe. Fakih Jundu, Jaji Kiongozi Mstaafu (wa sita kushoto), Bw. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (wa kwanza kulia), Bi. Enziel Mtei, Katibu, Msaidizi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Bw. Mapunda, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (wa pili kulia) na Bi. Georgina Mulebya, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, picha hiyo ilipigwa mara baada ya zoezi fupi la kuwapongeza waliokuwa Wajumbe wa Tume hiyo kwa kustaafu na kupandishwa cheo iliyofanyika katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu, Mahakama ya Rufani (T), Dar es Salaam. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum kama pongezi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Jaji Kiongozi Mstaafu, Mhe. Fakih Jundu mapema leo, zawadi hiyo imetolewa kwake kwa kutambua mchango wake kama Mjumbe wa Tume hiyo ya Mahakama.
Mhe. George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimkabidhi zawadi maalum aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Jaji Frederick Werema ambaye pia alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, zawadi hiyo imetolewa kwake kwa kutambua mchango wake katika Tume hiyo kipindi alichokuwa Kamishna.
Mhe. Jaji Shaban Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) (kulia) akipokea zawadi ya pongezi kutoka kwa Bi. Georgina Mulebya, Kamishna wa Tume ya Utuumishi wa Mahakama, zawadi hiyo ilitolewa na Tume kwa Mhe. Lila kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), kabla ya uteuzi huo Mhe. Lila alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...