Mgeni Rasmi Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi. Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kushoto) na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Mkoani Tabora.

Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi ambao ni washiriki wa mafunzo yanayohusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano. Waliokaa ni Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (katikati) na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi pamoja na wawezeshaji wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (aliyekaa katikati) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo. Picha zote Na: Thomas Nyindo-Tume ya Mipango .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...