Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na wataalam wanaofanya  Mapitio ya Sera ya Afya kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA.

MAPITIO YA SERA YA AFYA YA MWAKA 2007.
Utoaji wa huduma za afya nchini una simamiwa na Sera ya Afya ya mwaka 2007. Dhumuni kuu la Sera hii ya Afya ya Mwaka2007, ni kuinua hali ya afya ya wananchi wote na hasa wale walioko kwenye hatari zaidi, kwa kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa Watanzania. Mpaka sasa, Wizara yangu inaendelea kutekeleza Sera hii katika kusimamia utoaji na upatikanaji wa huduma za afya nchini. Katika utekelezaji wa Sera hii, Wizara na Sekta ya Afya kwa ujumla imepata mafanikio mbalimbali. Mafanikio haya ni pamoja na:

  • Ongezeko la Vituo vya kutolea Huduma: Wizara imeendelea kuboresha huduma za tiba kwa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM). Katika utekelezaji wa Mpango huo,vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015, sawa na ongezeko la vituo 2,075. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini, Vituo 5,072 ni vya Serikali na 2,175 nivyataasisibinafsi.

  • Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka112 kwa kila vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi 81 kwa vizazi hai 1000 mwaka 2010. Aidha, Taarifa ya Kimataifa ya Septemba 2013, imeonesha kuwa Tanzania tumeweza kufikia Lengo la millennia namba 5, la angalau kuwa na vifo 54 kwa kila vizazi hai 1000, Tanzania iliweza kufikia lengo hilo kabla ya mwaka 2015..

  • VifovitokanavyonamatatizoyaUzazivimepunguakutoka 578 kwakilavizazihai 100,000 mwaka 2005 hadivifo 432 kwavizazihai 100,000 mwaka 2012 navifo 410 kwavizazihai 100,000 mwaka 2014. PiamatumiziyaUzaziwampangoyameongezekakutokaasilimia 20 mwaka 2005 hadiasilimia 27 mwaka 2010.
  •   Huduma za Chanjo: Serikali imefanikiwa katika kupanua wigo wa huduma za chanjo ambapo, kiwango cha chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2005 hadi asilimia 97 mwaka 2014. Kutokana na mafanikio katika chanjo, Wizara imefikia viwango vya kimataifa vya kutokomeza pepopunda kwa watoto wachanga mwaka 2012 na pia imeweza kudhibiti ugonjwa wa Polio.
  • Kusoma zaidi Bofya Hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...