Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe amesitisha shughuli za maandamano na mikutano  zilizokuwa zimepewa jina la UKUTA  na zilizopangwa  kufanyika Septemba 1, 2016 kwa kile alichodai hatua hii imekuja baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi mbalimbali kufanya hivyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,  Freeman Mbowe amesema  Viongozi hao wakuu wa kidini wamewaomba na kuwasihi katika vikao mbalimbali walivyokaa pamoja nao na kusema tunaheshimu viongozi hao. 
Mbowe amesema wanawapa muda wa wiki mbili au tatu ili waonane na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa na kuliepusha taifa na machafuko ya kisiasa. 
Pia amesema Viongozi wa Taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wamewasihi kuahirisha UKUTA kwa muda ili kutoa fursa kwa jitihada za mazungumzo na majadiliano kufanyika. 
"Sisi CHADEMA tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba na Sheria za nchi yetu. 
"Hata hivyo tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa zaidi haki za Watanzania ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yao" amesema Mbowe".
Amewatangazia viongozi wote  wa ngazi zote CHADEMA, pamoja na wanchama,wafuasi na Watanzania wote kuahirisha  mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hesabu. Leo mmewakwepa jwtz ambao wana aniversary. Baada ya mwezi mmoja mtakutana nao kwenye usafi.

    ReplyDelete
  2. Afadhali.

    ReplyDelete
  3. Dini dirisha la kutokea tu. Hapakuwa na maandamano yoyote. Kibano kilikubali. Tusidanganyane.

    ReplyDelete
  4. Mbona Jk hakuogopa mikutano na maandamano? Binafsi sioni busara wala ulazima wa kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano.

    ReplyDelete
  5. Hakuna cha UKUTA wala KIAMBAZA.

    ReplyDelete
  6. Nadhani ni wakati mwafaka wa muswada wa kupunguza nguvu za rais.

    ReplyDelete
  7. mikutano ya nini bwana, fanyeni kazi, na kwanini mshurutishe watu, achene hizo, siku hizi akili za kuambiwa changanya na za kwako. imekula kwenu. subirini 2020. tuacheni tufanye kazi bwana.

    ReplyDelete
  8. Muacheni Rais wetu atusaidie kuishi kwa utaratibu, mlilia sana mnataka Rais mkali, mmempata tena mnageuka, ama kweli walimwengu vigeugeu, sasa mnataka kuandamana ili iweje, tulieni mtuache atusaidie ili twende mbinguni Bwana, mnajua dhambi zilizidi sana, wizi, rushwa, viburi, majivuno, mbwembwe, makwazo, sasa hivi mnayaona tena hayo, kwishenei kabisa, kila mtu anamwona mwenzake binadamu. Heshima na adabu. upinzani si kupinga kila kitu mema myasifie. tulieni muone, mbona sisi watanzania hatulalamiki, ina maana nyie ndio mnaumia, au danganya toto? Muacheni Rais wetu afanye kazi.

    ReplyDelete
  9. Hata maandamano yasingekuwepo. Watu wanatafuta kipato na chakula watapoteza muda kuwafuata jamaa waloishaiba na kushiba. Tusidanganywe Bwana. Hata Oktoba 1 hakuna chochote. Watasingizia Mungu sasa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...