Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wengine pichani ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (kulia) na Gerald Hando.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akionyesha moja ya T-shirt wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaoangalia ni  waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na  kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaopokea ni   waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando.

KATIKA juhudi za kuendeleza sekta ya michezo nchini,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imekabidhi jezi za michezo kwa Uongozi wa Tamasha la Mziki Mnene na Vodacom ulioandaa tamasha mahusisi kwa timu mbalimbali zitakazoshiriki katika mpira wa miguu wa maveterani katika tamasha hilo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wakati wa tamasha hilo lililoandaliwana kituo cha EFM linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi ijayo chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
 Akiongea katika hafla ya kukabidhi  kwa uongozi huo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema Vodacom Tanzania inafurahi kudhamini tukio hili muhimu lenye lengo la kutoa burudani kwa jamii kupitia tasnia  ya muziki na michezo.

 “Vodacom tunafurahi kushiriki katika tukio hili la kuleta burudani kwenye jamii na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kudhamini  michezo na Sanaa kwa kuwa inaamini kupitia sekta ya michezo watanzania  wengi wanaweza kupata burudani wazipendazo na kupumzisha akili  pia kupitia tamasha hili wananchi  watapata fursa ya kupata na kununua bidhaa mbalimbali za mawasiliano kutoka Vodacom popotelitakalofanyika tamasha hili huduma zetu zitakuwepo na tutaendelea kudhamini  matukio ya burudani kwa ajili ya kuinua vipaji vya Sanaa na michezo kama ambavyo kwa sasa tunavyoendelea kudhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara na mashindano ya kucheza muziki wa dansi ya Dance 100%  na tuzo za wasanii ya EATV”Alisema.

Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo Mratibu wa tamasha hilo,Denis Sebbo amesema kuwa tamasha la muziki mnene mwaka huu, litafanyika kwa kipindi cha muda wa wiki 12  ambapo muziki utapigwa katika baa 12 za Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wasanii ambao watapamba tamasha hilo aliwataka kuwa ni Machupa,Msaga Sumu,Dula Makabila,Easy Man,Khalid Chokoraa,Mc KKoba,Shoz Dear,Peter Msechu,AT,Majid Migoma, Dogo Niga na Rublay.

Alisema tamasha la muziki mnene mwaka huu litaenda sanjari na kampeni ya NJE NDANI ambapo vipindi vinne  mbalimbali vya redio hiyo viratushwa  live  naaliwataka wapenzi wa michezo na burudani kuhudhuria  tamasha hili ambalo ni mwisho wa burudani  na  tayari limeishaanza kuwa gumzo ya jiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...