Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
VYUO vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi ambao hawapo vyuoni vinatakiwa kurejesha fedha hizo ndani ya Siku saba kuanzia leo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa vyuo hivyo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usaili, matokeo ya majaribio na matokeo ya mitihani pamoja na namba za akaunti za benki ambapo  mikopo hulipwa huko.

Profesa Joyce amaesema kuwa vyuo vikuu vinatakiwa kuwasilisha taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi kwa wakati ili kuiwezesha bodi ya mikopo kufanya marekemisho ya stahiki katika kumbukumbu zao ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.

Pia amesema kuwa hatu kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote watakaohusika kufanikisha malipo kwa wanafunzi ambao hawapo vyuoni.
Profesa Joyce amesema kuwa uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambazo zimelipwa kwa watu wasiostahili.

Pia wakuu wa vyuo(VCs Principals) wametakiwa kuweka mfumo wa sahihi uhakiki wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya Mikopo na wakuu hao watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaidi kuwa na udanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi kwa kuwa kunawanafunzi ambao hawakfanya mitihani na wengine wamefeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mkopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Warejeshe pesa zote na mianya yote izibwe na kanuni na taratibu mpya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...