Na Selemani Semunyu JWTZ.

Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ wamekabidhiwa Medali za Dhahabu ikiwa ni sehemu ya kunyakua ubingwa wa Mchezo huo katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki yaliyofanyika Kigali Nchini Rwanda,Mbali na zawadi hiyo Mchezaji Nasra Suleiman wa Timu hiyo ya JWTZ ameshinda tuzo ya Most Valuable Player (MVP) na hivyo kuongeza shangwe kwa T imu ya Tanzania.

Akitoa tuzo hizo ni Mkuu wa Jeshi la Anga la Rwanda Brigedia Generali Charles Karamba alisema katika mashindano haya ambayo ushiriki ndio jambo muhimu kwani sote ni washindi lakini wapo waliofanya vizuri wanaopaswa kupongezwa.

Alisema Katika Netball Tanzania imefanya Vizuri ikifuatiwa na Uganda kisha Kenya hivyo ni nafasi nzuri kuwapongeza waliofanya vizuri zaidi na pia waliofanya vibaya ili kujipanga upya katika mashindano yajayo.
Akizungumza na Waadishi wa habari mkuu wa Msafara wa Timu za Tanzania na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Timu za Tanzania Brigedia Jairos Mwaseba aliipongeza Timu hiyo na kuda ushindi huo waliutarajia kutokana na maandalizi yaliyofanyika.

Kwa upande Mlinzi wa Timu hiyo Joyce Kaira na Mshambuliaji Mwanaidi Hasan walisema wamefurahi kwani waliupoteza ubingwa huo mwaka jana.
Naye Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema maandalizi mazuri yaliyofanywa na Jeshi ndio siri ya ushindi huo sambamba na Nidhamu na kujituma.

Timu hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kombe katika sherehe za ufungaji wa mashindano hayo katika uwanja wa amahoro ambapo mchezo wa mwisho wa Soka kati ya Rwanda na Tanzania utachezwa na kuamua mshindi wa mchezo huo.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ Dorita Mbunda akivalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu hiyo muda mchache baada ya kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ kikiingia kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi)
Mkuu wa Msafara wa Timu ya Tanzania Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba (katikati) akiongea na Mchezaji Nasra Suleiman aliyeshika Tuzo ya MVP na mwanaidi Hassan mara baada kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda.
Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ Nasra Suleiman akipokea kikombe cha MVP na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya Timu yake pia kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Selemani Semunyu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...