Na Raymond Mushumbusi - WHUSM 

Wadau wa Michezo nchini wameshauriwa kujenga viwanda kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.

Ushauri huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizindua channeli mbili za Michezo za Kampuni ya king’amuzi cha TING.

Naibu Waziri Anastazia alisema kuwa kwa kupitia uwekezaji huo kutasaidia kuinua sekta ya michezo nchini pamoja na kuondokana na changa moto ya vifaa vya michezo jezi za michezo,mipira na vifaa vinginevyo.

“Tuunge mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwekeza katika viwanda vitakavyotengeneza vifaa vya michezo” alisema Mhe. Anastazia

Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa vifaa vya michezo nchini kwani vifaa vingi vya vinatoka nje ya Tanzania hivyo huuzwa kwa bei ya juu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Frenandes ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa Michezo nchini katika kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Chaneli za Michezo zilizozinduliwa katika Kingamuzi hicho ni ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 ambazo zitakuwa zikionesha michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.    

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata utepe kuashiria uzindua wa Channeli mbili za michezo ambazo ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.


aibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Michezoalipokuwa akizindua uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt .Veron Fernandez akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo nchini Agosti 28,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.Picha na 
Raymond Mushumbusi - WHUSM
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...