Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
VIONGOZI wa madereva waendesha bodaboda mkoa wa Dar es salaam wamewaasa wanachama wao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote. 

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti waendesha bodaboda kutoka Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam Almano Mdede wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utendaji wao wa kazi za kila siku. 
Viongozi hao wamesema kuwa wanaimani na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika uongozi wake kwa dhamira yake ya kuwatumikia Watanzania na kuwataka madereva bodaboda wenzao kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma ya usafiri katika maeneo yao.
“Ninawaomba wanachama wa chama cha madereva bodaboda mkoa wa Dar es salaam tutambue kuwa sisi ni wafanyabiashara kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Tafadhali tumpe sekunde aweze kutekeleza aliyoahidi kwa Watanzania” alisema Mdede.
Aidha, Mdede alisema kuwa waendesha bodaboda hao ni wafanyabiashara kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni vema wafanye biashara kulingana na leseni zao.
Naye Mjumbe wa madereva wa bodaboda kutoka Kinondoni Oscar Waluye alisema kuwa waendesha bodaboda ambao ni wanachama katika umoja wao ni wale waliosajiliwa na kufanya biashara kwa kuzingatia leseni zao ambapo utambulisho wao unatokana na namba zao za pikipiki ambazo zimesajiliwa kwa “plate number” nyeupe na namba za usajili zimeandikwa kwa rangi nyeusi.
Aidha, madereva hao wamewaomba madereva bodaboda wenzao nchi nzima kupitia viongozi wao kuendelea kushirikiana na Serikali ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na familia zao na taifa kwa ujumla.
 Mwenyekiti wa  Muungano wa Vyama vya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam Bw. A. Leonard Mdede (wapili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waendesha Bodaboda kutojihusisha na mamandamano ya UKUTA leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Michael Maiko, Mapinduzi Mpema na Said Kagambo.



Katibu wa  Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni (KIDITIMA)  Oscar Waluye (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu waendesha Bodaboda kutojihusisha na mamandamano ya UKUTA uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni  Mwenyekiti wa  Muungano wa Vyama vya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam Bw. Mdede,Said Kagambo,Mapinduzi Mpema na Michael Maiko ambao ni viongozi wa vyama hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...