Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wasanii wapenda Amani nchini, Asha Baraka akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tamko lao la kuungana pamoja kupinga Maandamano ya UKUTA, Septemba 1.  
Mwenyekiti wa Umoja huo, Steven Mengere (Steve Nyerere) akizungumza juu ya kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika  Septemba Mosi kote nchini.
Mwanamziki na Malkia wa Nyimbo za Taarab, Khadija Kopa akizungumza katika mkuatano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Ally Choki akizungumza katika Mkutano wa Kupinga maandamano ya UKUTA jijini Dar es Salaam leo.

WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere amesema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka amesema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.
Amesema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
Hatahivyo ameomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Extremism in defense of liberty is a vice. Exremism is always a vice. Use of deadly force against peaceful demos is extremism. The wise man who said extremism was no vise was wrong. Cant justify sheding blood of one to protect the blood of your choice. You have to protect blood of all people even of those who anoy you. That is why being a leader is difficult. Cant do what commons do.

    There almost has not been a right that has been given to folks for free in the world. People have to take it and sacrifice for it. Freedom of all kinds, of speech, of movement, .... are God given. Cant take it. Prosecute them for bad mouths but dont kill them for kuandamana. Kuandamana is not murder nor war crime. Why kill em.

    They tempt you to commit a deadly mistake and you give in. Busara na hekima za wazee wa nchi zisinyamaze

    ReplyDelete
  2. Nyerere kajitahidi kifogo. Wengi wanatoa ushauri kwa chadema. Ushauri mzuri. Lakini wamesahau makusudi kushauri serikali kutoa maelekezo yasiyopingana na katiba. Serikali ikitaka jambo ambalo kikatiba si zuri basi ifuate taratibu kwa kuweka mswada bungeni na kufanya sheria.

    Serikali irekenishe kipengele cha katiba kinachoruhusu mikutamo ya siasa na maandamano ili atakayekiuka basi sheria imuumize. Sasa hivi kuna utata haijulikani kati ya serikali na chadema ni nani anafata katiba. Ila katiba iko wazi kwenye kuruhusu siasa na mikutamo na maandamano.

    Na chadema nanyi pendekezeni miswada itayowapa nguvu ya kuafanya mtakayo. Kutoka bungeni ni kinyume cha mkataba wa kazi mlioomba ya kuwasemea wananchi.

    ReplyDelete
  3. Mutual natural peace not tank peace. Tank peace protects few while majority are deprived of alot and if they ask for their dues they are acused of disruption of gun peace and the gun goes to work. Guns dont kill people, people protected by guns kill unprotected people.

    ReplyDelete
  4. mbona JK aliruhusu mikutano na maandamano na ameondoka nchi ina amani? wengi tunaangalia tulipoangukia badala ya kuangalia tulipojikwaa.

    ReplyDelete
  5. Wangewaacha waandamani wasikize wanachokiongea. Ilimradi polisi walinde amani siku hiyo...Kuwanyima ni kutoruhusu watu kujieleza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...