Mkuu wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Martha Haule akitoa taratibu zitakazofuata wakati wa ugawaji wa zawadi kwa washindi wa wa shindano la Jijenge na Twiga Cement lililofanyika katika kiwanda hicho. 
Mshindi wa mashine ya kufyatulia tofali kwa kutumia saruji, Hamza Juma Mtuli kutoka Dodoma akijaribisha mashine hiyo kama iko imara mara baada ya kukabithiwa cheti cha ushindi.
Mshindi wa Mifuko ya saruji 400,  Sweya Lufuta(katikati) akieleza jinsi kieleza jinsi gani alivyoshinda zawadi hiyo ya mifuko ya simenti 400 kwenye promosheni ya ‘Jijenge na Twiga Cement’ iliyochukua takribani mwenzi mzima.
Meneja Usambazaji wa Twiga Cement, Tumain Joseph (kulia), akimkabidhi cheti mshindi wa mifuko  ya saruji 600, Revocatus Mombeki katika promosheni ya ‘Jijenge na Twiga Cement’ iliyomalizika leo
Picha ya Pamoja

Na Moi Dodo 
KAMPUNI inayozalisha saruji ya Twiga, imekabidhi mashine mbili za kufyatulia tofali za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 15, kwa washindi wawili wa shindano la JijengenaTwiga katika hafla iliyofanyika leo siku ya ijumaa. Aidha, kampuni hiyo imekabidhi washindi wengine watatu jumla ya mifukoya saruji 1200, ambao walijishindia katika droo ya nne ya shindano hilo ambalo lilianza mwishoni mwa mwezi wa Julai mwaka huu.

Akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Simon Delens alisema promosheni hiyo imelenga kuwawezesha watanzania kujijenga kiuchumi na kijamii kupitia bidhaa za kampuni hiyo. Delens aliwataja washindi hao kuwani Paskali Karani kutokaArusha, na Hamza Mtuly kutoka Dodoma ambao wamejishindia mashine za kufyatulia tofali za saruji, ambazo zilitolewa kupitia shindano hilo la Jijenge naTwiga Cement.

“Leo tumefaniki shandoto za washindi wetu hao, kwa kuwapatia stahiki zao. Pia aliongezea kwa kusema nawapongeza washindi wa mashine na nawasihi wazitumie katika kuanzisha vituo vyao vya kibiashara. Kwa wale walioshinda mifuko ya cement nao wakaitumie kujiendeleza na zaidi yayote watakwenmshindi wa mashine ya kufyatulia tofalida kutimiza ndoto zao walizokuwa wakiziota kabla ya kucheza promosheni hii,” alisema Delens.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti, washindi hao wa mashine hizo walisema kuwa ilikuwa ni bahati na kila mmoja hakuamini alipopigiwa simu na kuambiwa kuwa amekuwa mshindi. “Sikuamini kwa kweli. Ilikuwa ni bahati ambayo hadi sasa ninapokabidhiwa cheti cha ushindi, ndiyo naamini. Sikuwahi kufikiria kuwa nitashinda zawadi kama hii wakati naanza kushiriki,” alisema Mtuly. Kwa upande wa washindi wa mifuko, Delens aliwataja washindihao kuwani Salum Ismail aliyeshinda mifuko 200, Sweya Lufuta aliyejishindia mifuko 400 na Revocatus Mwombeki ambaye alishinda mifuko 600.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baadaya kukabidhiwa zawadi zao, Mwombeki ambaye alishinda mifuko 600 alisema kuwa ushindi huo nifaraja kwake na atautumia kuongezea mtaji wake. “Mimi ninafanyashughulizaufundimkoaniiMwanza. Zawadi hii ya mifuko 600 ya cement ya Twiga nitaitumia kujenga nyumba ya kuishina kuanzisha mradi wa kufyatua matofali ambayo itakuwa biashara itakayoniongezea fedha zaidi. Nimefurahi kupata ushindi huu na Twiga wameniwezesha, hivyo kila kitu kimebaki kwangu,” alisema Mwombeki. 

Kwaupande wake, Lufuta aliyeshinda mifuko 400 alisema atatumia zawadi hiyo kukamilisha nyumba yake ya kuishi ambayo itakamilika mapema kuliko alivyopanga.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...