1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo akiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena Kiongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaotoka Dar es salaam kwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua ambapo wageni mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa wako mkoani humo kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo nadra kutokea duniani.
2
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi wakiagana na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na Antonio Nugas Mtembezi kutoka Clouds Media Viongozi wa Msafara wa Watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
3
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo vya habari hapa nchini wakiendelea na kazi yao wakati msafara huo ukiondoka jijini Dar es salaam.
4
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Mh. Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devotha Mdachi wakielekea kwenye gari kwa ajili ya kuwaaga baadhi ya watalii wa Ndani na waandishi wa habari wanaokwenda Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua wakitokea jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Good job uncle Tom.
    with love from CA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...