WATANZANIA waaswa kuhamasika kwa wingi kwenda Lujewa Mkoani Mbeya kuona kupatwa kwa jua mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Philip Chitanga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa tukio hili hotokea kwa nadra sana mkoani humo.

Amesema kuwa watalii wa mataifa mengine wajitokeze kwa wiki kwenda kushuhudia tukio hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Philip Chitanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kuhusiana na watanzania wajitokeze eneo ambalo litapatwa na jua Lujewa Mkoano Mbeya. Amesema kuwa Tukio hilo hutokea kwa nadra sana hapa nchini sasa ni wakati wa watanzania kuona tukio hilo la kupatwa kwa jua. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko katika bodi ya Utalii(TTB) na kushoto ni Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii(TTB)wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Philip Chitanga jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Philip Chitanga akizungumza na kusisitiza watanzania na watalii mbalimbali kujitokeza kwa wingi zaidi kwenda kushuhudia tukio la Kupatwa kwa Jua Lujewa Mkoani Mbeya.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona story haielezi hilo tukio litakuwa lini? Mtu ataenda tu Lujewa hata kesho??? Naomba muwaulize TTB kisha muweke tarehe ya tukio halisi.
    Thnx.

    ReplyDelete
  2. Ni tarehe 28 kesho I think so

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...