Watu wenye ulemavu 19 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva  ya mwezi mmoja kutoka katika shule ya udereva ya Nyato’s iliyopo Majohe Manispaa ya Ilala na Mkuu wa Usalama mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi  (ASP)Peter Mashishanga  huku akiwataka kabla ya kuingia barabarani wahakikishe wanakwenda kufanyia majaribio ili kuweza kupata leseni.
Akizungumza Dar es Salaam  katika Hafla  fupi ya kugawa vyeti hivyo iliyofanyika chuoni hapo Majohe Wilayani Ilala. Mashishanga alisema kuwa anaamini watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wengie hususani wale ambao hawafuati sharia na kuamua kuingia barabarani pasipo kupata hata mafunzo wala leseni.
“Leo hii mmepata vyeti hivi ni hatua muhimu ila sasa kabla hamjaaza kuendesha lazima mje pale Polisi katika Ofisi za Kikosi cha Usalama barabarani ili kuweza kujaribiwa na wakufunzi wetu tayari kwa kupata leseni itakayowapa ruksa ya kutumia vyombo vyenu vya moto”alisema
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa namna anavyoshirikiana na Kikosi hicho huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na pia alimweleza Mkuu huyo wa Usalama wa mkoa wa kipolisi kuwa shule yake imetoa ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli.
 Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi  wa Polisi (ASP)Peter Mashishanga akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya udereva  ya mwezi mmoja kutoka katika shule ya udereva ya Nyato’s iliyopo Majohe Manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato ya udereva ya Nyato’s iliyopo Majohe Manispaa ya Ilala akimkaribisha Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi  (ASP)Peter Mashishanga kuongea machache na wahitimu hao leo jijijni Dar es Salaam.
 Mkuu wa kItengo cha Elimu kwa Umma Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Mossi Ndozero akitoa eliu kwa wahitimu wa mafunzo ya udereva  ya mwezi mmoja kutoka katika shule ya udereva ya Nyato’s iliyopo Majohe Manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi (ASP) Peter Mashishanga 
 Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi (ASP)Peter akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu hao Bw. Mussa Nyahove leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi  (ASP)Peter Mashishanga   akiwa katika picha ya Pamoja na wahitimu wa mafunzo ya udereva  ya mwezi mmoja kutoka katika shule ya udereva ya Nyato’s iliyopo Majohe Manispaa ya Ilala leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...