Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasilisha muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mapema jana tarehe 24 Agosti 2016 katika ukumbi wa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali mjini Dodoma zinakoendelea  
Kamati mbalimbali za Bunge. Kamati hiyo ya Bunge ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba (MB). Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano wa nne wa Bunge utakaoanza tarehe 6 September 2016.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongoza mkutano huo wa Kamati wakati wa kuwasilisha  muswada wa kutunga Sheria ya wanataaluma wa kemia mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge. Kulia kwake ni Naibu waziri Wizara hiyo Dkt Hamisi Kigwangwalla
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel V. Manyele (Katikati) akifuatilia mkutano huo wa Kamati mjini Dodoma
Sehemu ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...