MJUMBE  wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa  (Nec) Yusuph Mrisho Kikwete amekuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Middle Star Saloon Foundation iliyopo Wilaya ya Bagamoyo,Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani  hapo Leo,Mjumbe huyo wa kamati kuu Nec ambaye aliongozana na Katibu msaidizi wa wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Salumu  Mtelela amesema kuwa  wameamua kuunga mkono kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

“Nimefurahishwa sana kuona vijana wanaamua kujiajiri haswa katika kipindi hiki ambacho nchi mbalimbali duniani zinapitia changamoto za ukosefu wa ajira kutokana na ongezeko la watu, kilichonifurahisha zaidi licha kuwa saloon ni ya kisasa lakini huduma zake za chini mtu yoyote anaweza kumudu,”amesema  Kikwete.

Kwa upande wake  Mkuu wa habari na Masoko wa Foundation hiyo,James Mbuligwe amesema kuwa lengo kubwa ni kufungua Saloon katika maeneo mengi ndani na nje ya mkoa ili vijana watumie nafasi ya kujiajiri kupitia kunyoa nywele .

“Saloon moja inachukuwa zaidi ya watu 10, hivyo ukiwa nazo 10 unakuwa umesaidia vijana zaidi ya 100 kuajiriwa ndio maana tumeamua kufungua mradi huu na leo tutatoa huduma bure kwa siku nzima ili kila mmoja apate ofa hii lengo letu ni kupunguza  tabia hatarishi zilizokuwepo katika jamii yetu zikiwemo utumiaji wa Madawa ya Kulevya ,Ukahaba na Ujambazi.

Mbulingwe amesema kila mtu anawajibu wakulinda amani ya nchi na  kijana akikosa kitu cha kufanya ni rahisi kuingia kwenye makundi mabaya.

Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Yusuph Kikwete katikati akiwa na Katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Pwani Salumu Mtelela kushoto, Mkuu wa Habari na Masoko wa Middle Star Saloon Foundation  James Mbuligwe kulia pamoja na wafanyakazi wa saloon hiyo
Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Yusuph Kikwete akipatiwa huduma na moja ya vinyozi wa Saloon aliyoizundua leo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Yusuph Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Habari na Masoko wa Middle Star Saloon Foundation James Mbuligwe wakati akiwasili kwenye saloon hiyo leo Wilaya ya Bagamoyo, Kushoto ni Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Pwani Salumu Mtelela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...