·        Zaidi ya wateja wa Airtel 350,000 wanufaika na mpango wa Wazazi Nipendeni
Airtel Tanzania yajivunia kufikia ujumbe mfupi (sms) upatao 20,0000 bila gharama yoyote kwa wateja zaidi ya 350,000 kwa ushirikiano na mHealth  Tanzania kupitia huduma yao ya Wazazi Nipendeni (Afya ya uzazi na mtoto) tangu kuzinduliwa 2012. Wateja wa Airtel waliojiunga na huduma hii wamekuwa wakipokea ujumbe mfupi wa bure wenye taarifa muhimu za afya na kupata ushauri kwa wamama wajawazito na wenye watoto wadogo Tanzania nzima.
Kubainisha hayo Mama lishe Aneth Pius (30) kutoka Dar es Salaam alisema, “ninamimba ya miezi 7 na nimekuwa napata ujumbe mfupi wa tarehe za kutembelea zahanati na umuhimu wa kufanya maadalizi mapema kabla ya kujifungua na pia athari za kutojiandaa unapokaribia kujifungua. Naishukuru sana Airtel na mHealth kwa huduma hii inayonisaidia katika kipindi hiki cha ujauzito”.
Miongoni mwa wateja 350,000 wa Airtel waliojiunga na huduma hii, 31% ni wanawake wajawazito, 18% ni wazazi wenye watoto wachanga, 17% ni wasaidizi wa afya na 34% ni wateja waliojiunga kupata taarifa mbalimbali za afya.
Akizungumzia hilo, Meneja huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi   alisema, “Airtel inajivunia kuwa kampuni ya simu ya kwanza kushirikiana na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika mpango wa Wazazi Nipendeni (Afya uzazi na mtoto) uliozinduliwa 2012. Kutokana na kuenea kwa mtandao wetu nchi nzima na wateja zaidi ya million 11 tulitambua umuhimu wetu katika kuwezesha upatikanaji wa taarifa za afya kwa jamii”.
Bayumi aliongezea akisema tunatamani kuona watu zaidi wakinufaika na huduma hii kupitia mtandao wetu na tunaendelea kuhakikisha tunatoa huduma hii bure kabisa kwa wateja wetu nchi nzima.

Huduma hii inasimamiwa na mHealth Tanzania ikishirikiana na washirika mbalimbali duniani. Njia ya kutoa taarifa za afya kwa ujumbe mfupi (SMS) imetambuliwa kuwa moja ya huduma bora nne za kutoa taarifa za afya duniani kwa mwaka 2014 na GSMA , Global Mobile Awards Committee, na moja kati ya huduma 6 zitokanazo na ubunifu wa kimtandao kwa 2016 na GSMA , Global Mobile Awards Committee.
Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi Airtel inavyoendelea kusaidia kutoa elimu ya afya kwa wanawake wajawazito na wenye watoto nchini Tanzania, kwa kupitia namba maalumu inayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma inyowapatia taarifa mbalimbali za afya ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel wakishirikiana na mHealth Tanzania na washirika wengine chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...