Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi
Na May Simba-MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Bonanza la Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambalo litafanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shimiwi. Bw. Moshi Makuka, bonanza hilo litafanyika tarehe 10, Septemba mwaka huu katika uwanja wa Taifa (Uhuru) kuanzia saa 12:30 asubuhi.

“Bonanza litawashirikisha watumishi wote wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salam” alisema ndugu Makuka.

Aidha Bw. Makuka alisema kwamba bonanza hilo ni maandalizi ya michezo ya Shimiwi ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 14 mpaka 27 Octoba mwaka huu.

Michezo ya mwaka huu ina lengo la kuunga mkono agizo la Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli la kuhamishia Makao Makuu yake mkoani Dodoma.

Mbali na hayo Bw. Makuka alisema michezo hiyo itawapa fursa watumishi wa umma kufahamu mazingira na kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kuhamia mkoani humo

Bw. Makuka aliongeza kwamba walipanga michezo hiyo kuanza Octoba 14 ili kuadhimisha kumbukumbu muhimu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere na kuenzi agizo lake la Serikali kuhamia Dodoma linalotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

“Michezo ya mwaka huu itaanza na ibada maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa na kumtakia afya njema Mhe. Rais Dkt. John Magufuli sanjari na kushiriki upandaji miti katika maeneo yatakayopendekezwa na Serikali ya mkoa”aliongezaBw. Makuka.

Michezo ya Shimiwi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaunganisha wafanyakazi wote na kuimarisha afya zao ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...