Mhe. Dkt. Mahadhi J. Maalim, akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Fouad Alghanim, Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim. Kushoto kwa Mhe. Dkt. Mahadhi ni Bw. Sami M. Al-Farhan, Makamu Wa Rais wa Umoja huo wa Makampuni ya Fouad Alghani anayeshughulikia masuala ya uwekezaji wa Kimataifa na mwanzo upande wa kulia ni Bw. Iman Njalikai, Mkuu wa Masuala ya Utawala katika Ubalozi wa Tanzania Kuwait.
Katika picha Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akiwa katika mazungumzo na Bw. Fouad Alghanim, Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim. 

 Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim, unajumuisha zaidi ya Makampuni ishirini ambayo yanajihusisha na masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, nishati, mafuta na gesi, usafirishaji, miundombinu, biashara ya magari, masuala ya anga na ndege, mawasiliano, ujenzi wa makazi ya kisasa, masuala ya ulinzi, utalii na afya.


Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti huyo alieleza matarajio yake juu ya ziara atakayofanya hivi karibuni kutembelea Tanzania ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana. Mwenyekiti huyo alimfahamisha mheshimiwa Balozi kuwa licha ya kutokuwa na shughuli za kiuchumi nchini Tanzania, Umoja huo unatekelezaji miradi mbalimbali katika nchi za jirani za Uganda, Rwanda na kwingineko. Aliongeza kuwa, Umoja huo una nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali Tanzania hususan miundombinu.

Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Maalim, alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuonesha nia ya kutembelea Tanzania na kuona fursa mbalimbali za uwekezaji. Vilevile, alimshauri kuangalia namna ambavyo Umoja huo unaweza kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta binafsi hususan katika suala la ujenzi wa makazi ya kisasa katika Makao Makuu mapya ya Serikali mjini Dodoma.

Aidha, Mhe. Dkt. Maalim, alipongeza kitendo cha Mwenyekiti huyo kuamua kufanya ziara Tanzania na kumuahidi kuwa Ubalozi wa Tanzania Kuwait upo tayari kutoa ushirikiano utakaohitajika ikiwepo kuwapatia taarifa muhimu kuhusu uwekezaji nchini Tanzania, pamoja kuwakutanisha na wadau muhimu katoka sekta binafsi na ile ya umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...