Mkuu wa Kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi akifafanua kuhusu matumizi ya kadi ya benki hiyo ya ‘Visa travel Money’ inayomwezesha mteja kufanya malipo mitandaoni kwa urahisi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini.
(Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha tuzo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliyopewa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania. Mkutano na waandishi wa habari umefanyika katika makao makuu ya benki hiyo mapema leo jijini Dar es salaam.
(Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha Tangazo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) lenye maelezo kamili kuhusiana na tuzo ya Visa waliyopewa hivi karibuni baada ya benki yao kuongoza katika miamala mitandao
Jitihada za BancABC katika ubunifu,kuendeleza na kufanikisha usalama wa miamala  matandaoni nchini Tanzania, imetambuliwa kwa tuzo ya Visa kuthibitisha ubora wa huduma yake mitandaoni.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi. Joyce Malai alithibitisha taarifa hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mapema leo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

“Tunafurahi kupokea tuzo hii licha ya ushindani wa masoko uliopo, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejidhatiti kuhudumia wateja wetu na kuwarahisishia kufanya miamala ya kifedha,” alisema Bi. Malai.

Aliongeza kuwa katika jitihada hizi za kuboresha miamala salama mitandaoni,  mtu yeyote anaweza kumiliki  kadi hii  ya Visa bila kujali kama anayo akaunti ya BancABC au la. Bi. Malai alifafanua kwamba kadi ya Visa ya BancABC ni rahisi kutumia kwani humhakikishia mteja ulinzi wa fedha zake na pia huondoa usumbufu wa kutembea na pesa taslimu.

Kadi hii inaweza kutumika kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha kama vile kulipia tiketi za ndege pia kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi, kulipa ada za shule na kujikimu kwa wanafunzi, mikopo na misaada kwa serikali na mengineyo.ili kupata kadi hii mteja anahitajika kuwa na  kitambulisho halisi na kisha kujaza fomu zinazopatikana katika tawi lolote la benki hii.

Aliongeza kwamba wateja wanaweza kuweka fedha kwenye kadi hiyo kwa kutumia huduma mbalimbali za kutuma pesa kama vile TIGOPESA, AIRTELMONEY au M-PESA pamoja na benki zingine zilizopo Tanzania.

“Tunaamini kwamba upekee wa huduma hii ndicho kilichowavutia wateja na hivyo kusababisha ushindi wa tuzo ya Visa,” alisema. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini alisema, kadi hiyo inaweza kutumika pia kwa fedha za mataifa mbalimbali kama Shilingi ya Tanzania, Dola ya Kimarekani, Euro na Randi ya Afrika Kusini.

“Licha ya kuwawezesha wateja kufanya biashara mitandaoni, Mteja anaweza kutumia pesa zake kwenye Visa ATM Zaidi ya 400 nchini au Visa ATM Zaidi ya 1.3milioni duniani kote.

 Zaidi ya hapo Visa inamawakala Zaidi ya 1000 Tanzania na mawakala Zaidi ya 35 milioni duniani kote. Kupata kadi hii tutumie barua pepe customercaretz@bancabc. com.
 
Atlas Mara iliinunua BancABC Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

Atlas Mara iliorodheshwa katika Soko la Hisa London, mwezi Desemba 2013. Ndoto za kampuni hii ni kuanzisha taasisi kubwa ya kifedha Kusini mwa Sahara kupitia uzoefu wake, umahiri na upatikanaji wa mitaji, ukwasi na uzalishaji fedha. Malengo yakiwa ni kujumuisha ujuzi wa taasisi za dunia nzima na mitazamo ya kina ndani ya Afrika, hivyo kusaidia kukuza uchumi katika nchi zinazo hudumiwa na Kampuni hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...