Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

UBALOZI wa china nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya china na wananchi wa china wametoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni mia moja kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea septemba 10 Mkoani Kagera.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa niaba ya Balozi wa China ambaye yupo likizo nchini China Dk. Lu Youqing, Naibu balozi wa china Zhang Biao alisema kuwa wamewatembelea wahanga wa tetemeko hilo na kujionea jinsi wananchi walivyohathirika.

"Ndugu zetu bado wanahitaji misaada kwani tetemeko limewaathiri sana kwani wapo waliopoteza makazi,waliojeruhiwa tumeona huzuni sana tulipoona hali hiyo,tunawapa poleni nyingi sana na tupo pamoja katika kipinfi hiki Kigumu"alisema Naibu Balozi huyo

Alivitaja vitu walivyotoa kwaajili ya wahanga wa tetemeko kuwa ni mahema,madawa,chakula na mablanketi.

Alisema Nchi ya china na Tanzania ni marafiki wanaoshirikiana katika sekta mbalimbali katika kujenga Taifa la Tanzania watazidi kusonga mbele.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu  baada ya kupokea msaada huo aliushukuru Ubalozi wa China kwa ushirikiano wao na kuguswa na maafa hayo ya tetemeko la ardhi kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.

Kijuu alisema kuwa msaada huo utawafikia walengwa kwa wakati na kamati ya maafa iliyoundwa itasimamia kwa karibu.amesema mpaka sasa kuna shilingi milioni 460 kwenye akaunti ya maafa ya kagera zilizotumwa  na wananchi wote Tanzania

"Ninawahakikishia kuwa msaada huu utawafikia walengwa na hakuna ujanja ujanja wowote utakaotokea,na misaada hii tutaanza kuwagawia walengwa walioathirika zaidi kama waliopoteza makazi,wazee na wajane"alisema Kijuu.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meje Jenerali mstaafu Salimu Kijuu akimshukuru Naibu Balozi wa China Zhang Biao baada ya kupokea msaada kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi
 Baadhi ya Madaktari wa kichina waliokuja bukoba kutoa huduma za matibabu kwa wahanga wa tetemeko la ardhi wakiwa kwenye picha ya pamoja. 
 Sehemu ya misaada iliyotolewa na serekali ya china kwa wahanga wa tetemeko Mkoani Kagera
 Lori lililoleta msaada wa serekali ya china Mkoani Kagera kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SHESHE.
    Kweli hawa ni marafiki. Vipi wale wanaotufundisha demokorasi hawajasikia hii shida?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...