Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Majid Mwanga amekemea na kuvipiga marufuku vitendo vya baadhi ya askari mgambo wenye  tabia ya kujihusisha na upitishaji na uingizaji wa  biashara za magendo na badala yake amewataka kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao  kwa lengo la kuweza kudumisha hali ya amani na  utulivu.

Kauli  hiyo imetolewa wakati alipokuwa akizungumza na askari mgambo pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kusherekea maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambayo yalikwenda sambamab na zoezi la ufanyaji usafi katika mitaa mbali mbali ya Wilayani  Bagamoyo ambayo pia yaliwajumuisha  wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.

Mwanga alibainisha  kwamba askari wanatakiwa kuwafichua wale wote ambao wanajihusisha na biashara hizo,ambazo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia fukwe za bahari ya hindi  kinyume na sheria na taratibu na kupelekea kuikosesha  serikali kukusanya  mapato kama inavyotakiwa kutokana na watu wachache kukwepa kulipa kodi.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiendesha trekta kwa ajili ya kupakia takataka wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya jeshi la wananachi Tanzanaia (JWTZ) ambapo aliwaongoza wananchi wa bagamoyo kufanya usafi katika mitaa mbali mbali.

“Mbona mnavusha wahamiaji haramu, mbona mnaingiza sukari za magendo,mbona mnashiriki kuvusha tairi za magendo na cha kushangaza hamtuambii lolote, kwa hiyo mimi ninachowaomba tabia hii sio nzuri na kitu kikubwa ni kushirikiana bega kwa began a jeshi la Polisi ii kuweza kuwafichua wale wote ambao wanafanya biashara hizo za magendo,”alisema Mwanga.

Mwanga alisema kwamba kwa sasa wataweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuweza kufanya msako wa mara kwa mara katika fukwe za bahari, ili kuweza kuhakikisha kwamba wale ambao wanajihusiha na biashara hizo zamagendo wanakamatwa na wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Katika hatua nyingine Mwanga alisema kwamba katika mkuhakikisha Wilaya ya Bagmoyo inakuwa na mazingira masafi muda wote wameweka faini ya kisi cha shilingi elfu hamsini kwa mtu yoyote atakayebainika anatupa taaka ovyo na kuongeza kuwa kuna program maalumu ambayo itazinduliwa na kushindanisha kata kwa usafi na washindi watapatiwa pikipiki kwa maafisa tarafa na watendaji.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiwa na baadhi ya askari mgambo wakati wanafanya usafi katika maadhimisho ya jeshi la wananci wa Tanzania (JWTZ).

Kwa upande wao baadhi ya askari mgambo  akiwemo Frank Mwaisame pamoja na Hamis Ramadhani  hawakusita kuelezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuiomba serikali kuwangalia kwa jicho la tatu katika suala zima la maslahi yao kwani wanafanya kwazi kwa kujitolea.

Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo  Erica Yegella mewaasa wakinamama wanatumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuweza kuleta chachu ya maendeleo pamoja na kuwaasa kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepukana na magonjwa ya  mlipuko.

Reha Mita ni  Kaimu mshauri wa mgambo Wilaya ya Bagamoyo pamoja na  Mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Bagagamoyo  Adam Maro ambaye ni mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya ya Bagamoyo walisema askari wanapaswa kuwa wazalendo na nchi yao ili kudumusha amani iliyopo. na hapa walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na maadhimisho hayo.

KATIKA kusherekea maadhimisho hayo ya miaka 52 ya Jeshi la wananzhi wa Tanzania (JWTZ)  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ameongoza zoezi la kufanya usafi kwa kuamaua kuendesha mwenyewe gari la kubebea  takataka  na kupita katika mitaa mbali mbali jambo ambalo liliweza kuwa ni kivutia kikubwa kwa wananachi. NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...